American British Academy
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
ABA Oman | |
Ilianzishwa | Mwaka 1987 |
Aina ya shule | Ya Kibinafsi & Kimataifa |
Msimamizi wa shule | Mona Nashman-Smith |
Jiji na nchi iliyopo | Muscat, Oman |
Waliojiunga | ¬ wanafunzi 720 |
Nembo | Nyoka |
Shule ya American-British Academy, ilianzishwa mnamo Septemba 1987, iko katika mji wa Muscat, Oman, na ni moja kati shule za kimataifa zilizoanzishwa kwenye kanda la Uarabuni. Ni shule ya kibinafsi isiyo yenye kutoa faida; ambayo wanafunzi hawalali hapo. Inafundisha shule ya msingi na sekondari kwa lugha ya Kiingereza wa kigeni waliohamia mjini Muscat. Ikiwa na wanafunzi watokao nchi zaidi ya 60 mbalimbali kwenye jamii ya shule iliyo na wanafunzi 720, ABA inakuza ubora kielimu ndani ya muktadha wa kuheshimu na kuelewa utamaduni. Wanafunzi wenyewe hutoka nchi mbalimbali duniani kote na hakuna kabila iliyo na watu wengi zaidi kuliko nyingine.
ABA ina walimu wao kutoka mataifa 18 wanaofundisha kozi iliyo na changamoto na kutoa mkono wa kudumisha mazingira ya kimataifa ya mafunzo kwa wanafunzi. Walimu wengi huja kutoka nchi za Australia, Kanada, Uingereza, Marekani na New Zealand, lakini walimu kutoka nchi za Amerika ya Kusini, Mashariki ya Kati, Asia, na Ulaya si wengi mno, lakini wote huleta muktadha wa kimataifa katika shule hii.
ABA inatambulika kikamilifu na vyama vya Middle States Association of Colleges and Schools na European Council of International Schools. ABA pia ni "IB World School," iliyo na mamlaka ya kutoa International Baccalaureate katika shule ya msingi (Darasa 1-5), na International Baccalaureate kwa shule ya kati (Darasa 6-10), na diploma ya International Baccalaureate (Darasa 11-12).
Shule hii inajulikana kote kwenye Ghuba la Kiajemi kwa michezo, sanaa na mashindano ya ubunifu. ABA imekuwa mwenyeji wa mashindano mbalimbali ya michezo katika Ghuba na Mediterranean na pia ikafanya sherehe za michezo na sanaa [Academic Ganes and Junior and Senior Arts Festivals (EMAC)].