Anania wa Arbela (alifariki Arbela, leo Erbil, Iraki, 345) alikuwa Mkristo wa mji huo aliyeuawa katika dhuluma ya mfalme wa Persia Shapur II[1].

Kisha kufungwa, kwa amri wa mganga mkuu Ardisag, mara tatu alipigwa mijeledi kikatili hivi kwamba watesi wake, wakidhani ameshakufa, walimuacha amelala barabarani. Kumbe usiku waumini wenzake walimrudisha nyumbani ambapo alifariki dunia [2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Novemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.