Anastasi, Felisi na Digna

Anastasi, Felisi na Digna (walifariki Cordoba, Hispania, 14 Juni 853) walikuwa Wakristo wa Cordoba waliouawa na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu waliungama hadharani imani yao ya Kikristo [1].

Anastasi alikuwa padri, Felisi mmonaki na Digna bikira. Kwanza wanaume waliuawa kwa upanga, hatimaye Digna alikatwa kichwa kwa kuwalaumu waliowaua.

Taarifa zao ziliandikwa na Eulogi wa Kordoba[2] [3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 14 Juni[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/57220
  2. Latin writings of Eulogius pdf downloads at documentacatholicaomnia.eu
  3. Complete Works of Eulogius of Cordoba English translations of Eulogius' writings.
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri
  • Tolan, John, Medieval Christian Perceptions of Islam, New York: Routledge, 2000. ISBN|0-8153-1426-4
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.