Angellah Kairuki
Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (alizaliwa 10 Septemba 1976) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake manamo miaka ya 2010 – 2015, 2015 - 2020 [1].
Mwaka 2015 alipata kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kabla ya hapo, alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Katiba na Sheria. Kabla ya kujiunga na siasa, alifanya kazi kama mwanasheria katika sekta ya umma na binafsi.
Kapata elimu yake ya upili katika shule ya upili ya Kilakala 1991 – 1994, elimu ya juu ya upili katika Shule ya upili ya wasichana Zanaki 1995 – 1997. Alipata shahada yake ya sheria kutoka chuo kikuu cha Hill nchini Uingereza mwaka 1998 - 2001. Alipata Stashahada ya uzamili katika sheria Chuo Kikuu Cha Staffordshire kwa kushirikiana na mafunzo ya kati ya sheria 2001 – 2002. Alifanyakazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama atibu wa sheria na wakili kati ya mwaka 2004 na 2008. Kairuki alihamia sekta binafsi kama mkuu wa idara ya maadili, mwafaka na Utawala katika VODACOM Group PTY.
Tanbihi
hariri- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
Marejeo
hariri1. "Profile: Hon. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki". Parliament of Tanzania. Retrieved October 25, 2016.
2. Rose Athumani (December 11, 2015). "New lean Union cabinet unveiled". Daily News. Retrieved October 25, 2016.
3. "Case Studies: Angellah Kairuki". African Leadership Institute. Retrieved October 25, 2016.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |