Anisi wa Thesalonike
Anisi wa Thesalonike (alifariki 406 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kaskazini mwa Ugiriki kuanzia mwaka 383 hadi kifo chake [1].
Mapapa walimfanya makamu wao kwa Iliriko yote wakati wa kaisari Theodosi Mkuu.
Alitetea imani sahihi kuhusu umungu wa Yesu Kristo na ubikira wa kudumu wa Bikira Maria. Kwa ajili hiyo alisifiwa sana na Ambrosi [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Desemba[3].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |