Antioko wa Anastasiopoli

Antioko wa Anastasiopoli (alifia dini Anastasiopoli, Galatia, leo nchini Uturuki, 303 hivi) alikuwa Mkristo wa Ankara aliyeuawa kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian kama kaka yake Plato wa Ankara kabla yake[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini, pengine pamoja na Siriako ambaye inasemekana alijitangaza kuwa Mkristo aliposhuhudia muujiza uliotokea Antioko alipokatwa kichwa naye akauawa vilevile.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Julai[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.