Ateri
Mshipa wa ateri | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Ateri (pia arteri, kutoka neno la Kigiriki ἀρτηρία, artēria, kupitia Kiingereza artery) ni mshipa wa damu unaopeleka damu nje ya moyo wa binadamu na wanyama kadhaa. Hivyo ateri ni sehemu ya mfumo wa mzunguko wa damu.
Mshipa huu hubeba damu yenye oksijeni kutoka kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili. Mwili unatumia oksijeni kutengeneza nguvu. Ateri nyingi hubeba oksijeni, ila ateri pekee isiyobeba oksijeni ni Ateri ya mapafu.
Ateri zina safu tatu. Safu ya nje ni nene na inaundwa na tishu. Safu ya kati inaundwa na misuli, kwa hiyo ateri inaweza kupanuka au kusinyaa, wakati safu ya ndani inaundwa na seli ambazo zipo pia kwenye moyo.
Mshipa wa arteri hauwezi kuuona kwa macho tu, ila unaweza kuuona kwa kutumia kifaa kiitwacho hadubini.
Ateri muhimu
haririKuna aina mbili za arteri:
Arteri kuu (aorta)
haririAorta (au aota) ni ateri kuu kwenye mwili: inaanza kwenye ventriko ya kushoto ya moyo ambayo ina damu iliyobeba oksijeni kutoka kwenye mapafu.
Aorta ni mshipa mkubwa kuliko mishipa yote katika mwili wa binadamu.Mshipa huu hushukua damu yenye oksijeni kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili.
Mshipa huu hugawanyika katika mishipa midogomidogo iitwayo mishipa ya kapilari.
Arteri mapafu
haririArteri mapafu ni aina ya arteri inayosafirisha damu isiyo na oksijeni kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu.
Ateri ya mapafu ni ateri pekee
- isiyoungana na aorta
- inayobeba damu isiyo na oksijeni.
Picha
hariri-
Ufafanuzi wa ateri
-
Mwonekano wa ateri katika moyo
-
Mshipa wa ateri ya mapafu
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ateri kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |