Asbel Kiprop
Asbel Kiprop (amezaliwa mnamo 30 Juni 1989 wilayani Uasin Gishu) ni mkimbiaji kutoka Kenya ambaye mtaalamu katika mbio za mita 1,500. Kiprop alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2008 katika mbio za mita 1500, baada ya Rashid Ramzi kupimwa na kupatikana kuwa alikuwa ametumia madawa ya kulevya. [
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Men's Wanariadha | ||
Anawakilisha nchi Kenya | ||
Summer Olympics | ||
Dhahabu | 2008 Beijing | 1500 m |
African Championships | ||
Medali ya Shaba | 2008 Addis Ababa | 800 m |
All-Africa Games | ||
Dhahabu | 2007 Algiers | 1500 m |
Maisha ya Kibinafsi
haririKiprop anatoka katika kijiji cha Kaptinga, karibu Eldoret. Yeye ni mwana wa David na Julia Kebenei. Babake David Kebenei pia alikuwa mwanariadha, ambaye alishiriki katika Michezo ya All-Africa mwaka wa 1987 nchini Kenya na kumaliza katika nafasi ya nne katika mbio za mita 1500. Kiprop alianza kukimbia akiwa na umri wa miaka 13, wakati alikuwa katika shule ya Simat. Baadaye aliacha masomo ya sekondari ili azingatie mafunzo na mazoezi. Kiprop alikuwa anafanya mazoezi katika Kipchoge Keino High Performance Training Centre mjini Eldoret. Hata hivyo, alifukuzwa kutoka kambi mwaka wa 2009 kwa kuvunja sheria kwa kuleta mchumba wake kwa kituo hicho. Kakake mdogo Victor Kipchirchir Kebenei pia ni mkimbiaji wa mbio za mita 1500.
Ana urefu wa mita 1.88 na uzito wa kilogramu 62. Yeye kufanyishwa mazoezi na Jimmy Beauttah.
Alishinda tuzo la mwanaspoti anayeahidi wa mwaka, Mwaka wa 2007 katika tuzo za mwaka za Kenya Sports Personality.
Kiprop amesema jina lake la kwanza, Asbel, linamaanisha aliye na dhamiria.
Wasifu
haririMwaka wa 2007 ndio uliyokuwa mwaka uliyoanzisha mambo mazuri, kwani alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya kuvuka nchi (mbio za vijana) [18] na katika Michezo ya All-Africa (mbio za mita 1500). Alikimbia kwa wakati wake bora kibinafsi kwa kumaliza katika nafasi ya nne katika mbio za mita 1500 katika mashindano ya dunia ya mwaka 2007 katika mji mkuu wa Osaka.
Katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2008, Kiprop alishindwa kidogo tu na mwanariadha kutoka Bahraini Rashid Ramzi na kukosa medali ya dhahabu. ] Hata hivyo, Kiprop alipewa medali hiyo ya dhahabu baada ya Ramzi kupimwa na kupatikana kuwa alikuwa ametumia madawa ya kulevya ya aina ya CERA, Dutu lililokuwa limepigwa marufuku ambalo ni toleo mpya la linalojulikana kama EPO. Kiprop amesema kuwa hajafurahishwa na jinsi alibvyoshinda medali hiyo ya dhahabu.
Katika mashindano ya dunia ya riadha ya mwaka wa 2009 katika mji mkuu wa Berlin, Kiprop hakuwasisimua wengi wakati alimaliza katika nafasi ya nne kwa mara ya pili katika mbio za mita 1500 (miaka miwili awali katika mashindano ya dunia ya mwaka 2007 pia alimaliza katika nafasi ya nne). Kiprop pia alishiriki katika mbio za mita 800 lakini alibanduliwa katika nusu-fainali.
Majalio
haririMwaka | Mchuano | Ukumbi | Tokeo | Ziada |
---|---|---|---|---|
2007 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Mombasa, Kenya | 1 | Mbio za Vijana |
Michezo ya All-Africa | Algiers, Algeria | 1 | mita 1500 | |
Mashindano ya Dunia | Osaka, Japan | 4 | mita 1500 | |
2008 | Mashindano ya Kiafrika | Addis Ababa, Ethiopia | 3 | mita 800 |
Mashindano ya Kiafrika | Addis Ababa, Ethiopia | 4 | mita 1500 | |
Michezo ya Olimpiki | Beijing, Uchina | 1 | mita 1500 | |
Fainali za mbio za Dunia | Stuttgart, Ujerumani | 2 | mita 1500 | |
2009 | Mashindano ya Dunia | Berlin, Ujerumani | 4 | mita 1500 |
Ubora wa kibinafsi - Ya nje
haririUmbali. | Muda | Pahali | Tarehe | |
---|---|---|---|---|
mita 800 | 1:43.17 | Doha | 2009/05/08 | |
mita 1500 | 3:31.64 | Roma | 2008/07/11 | |
mita 3000 | 7:42.32 | Torino | 2007/06/08 |
Taarifa yote iliyochukuliwa kutoka IAAF profile. [1]
Marejeo
hariri- ↑ IAAF, Kiprop Asbel Kipruto biography: Absel Kiprop biography Archived 30 Januari 2010 at the Wayback Machine.
Viungo vya nje
hariri- IAAF wasifu wa Asbel Kiprop