Atanasia, Teodosia, Teotista na Eudosia

Atanasia, Teodosia, Teotista na Eudosia (walifariki Canopus, 31 Januari 311) ni wafiadini Wakristo wa Misri.

Atanasia alikuwa mjane, na hao watatu walikuwa mabinti wake. Waliuawa pamoja na Siro na Yohane waliokuwa wamekwenda kuwatia moyo kwa kusikia wamekamatwa.

Habari zao ziliandikwa na patriarki Sofroni wa Yerusalemu.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 31 Januari[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.