Gwantwa Ezekiel Grayson (Aunt Ezekiel) (alizaliwa jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba 1986) ni mwigizaji wa Kitanzania aliyejulikana kwenye uigizaji wa filamu 'Prison Revenge’, ‘Pumba Jungu La Urithi’ na ‘Eyes on Me’.

Aunt Ezekiel
AmezaliwaGwantwa Ezekiel Grayson
28th October 1986
Kazi yakeMwigizaji, mtayarishaji wa filamu,
Miaka ya kazi2000-hadi sasa

Baba yake alijulikana kama Ezekiel Grayson ambae alikuwa mchezaji bora wa timu ya mpira wa miguu Simba.[1]

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alimaliza elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Chanzige wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani.

Alianza Kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kawawa na alifikia kidato cha pili, na kurudi Dar es Salaam na kumaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makongo.

Baada ya kumaliza Sekondari ya Makongo alijiunga na mafunzo ya Kompyuta Amana, na alishiriki mashindano ya urembo na kuibuka Miss Mwanza 2006.

Maisha ya Ndoa

hariri

Mwaka 2007 alifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara Jack Pemba na kupata watoto watatu, ila baadaye akaoana na dansa Mosse Iyobo.

Viungo vya nje

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aunt Ezekiel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.