Baaziz
Baaziz, jina la sanaa Abdelaziz Bekhti, (alizaliwa 1963 huko Cherchell, kaskazini mwa Algeria ) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Algeria[1].
Maisha ya awali
haririIngawa anaishi Ufaransa, Baaziz ni mmoja wa waimbaji na watunzi wa nyimbo mahiri zaidi wa nchini Algeria. Baaziz alivutia mashabiki kwa wimbo wake wa kwanza wa "ya Hasrah kikount Esseghir" (kwa Kiingereza Once upon a time I was a kid ). Katika muda mwingi wa kazi yake alipigwa marufuku nyimbo zake kuchezwa kwenye redio na TV za Algeria.
Hata hivyo, wimbo wake uliompa mafanikio zaidi ulikua "Algeria My Love," ulimsababisha kutambuliwa maalum kutoka kwa Rais Bouteflika. [2] Na kukubalika na serikali ya Algeria, hata hivyo, kulidumu kwa muda mfupi. Uamuzi wake wa kuimba wimbo wa kuwashutumu majenerali wa Algeria, "Waili Waili," kwenye kipindi cha televisheni cha moja kwa moja licha ya onyo ulisababisha apigwe na kulaumiwa. [3]
Kazi
haririMwaka 2008 Baaziz alitangaza nia yake ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa Algeria . [4] Hata hivyo ugombea huo haukutimia na akatangaza kuwa hatamuunga mkono yeyote kati ya wagombea. [5]
Orodha ya kazi zake za muziki
haririMarejeo
hariri- ↑ "Les Enchanteurs ont accueilli Baaziz et sa valise de chansons engagées". web.archive.org. 2011-07-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-10. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
- ↑ "L'indépendence de Baaziz". Radio France Internationale. 28 Juni 2004. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2010.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Martin, Marie-Hélène (2008). Le Petit Futé Algérie. Petit Futé. uk. 131. ISBN 978-2-7469-2196-2.
- ↑ "Baaziz candidat à la présidentielle?". Jeune Afrique. 10 Desemba 2008. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2010.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "" Je ne soutiens aucun candidat à la présidentielle "". El Watan. 23 Machi 2009. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2010.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |