Kenneth Brian Edmonds[1][2] (amezaliwa 10 Aprili, 1959), anajulikana sana kwa jina lake la kisanii kama Babyface, ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na myatarishaji wa rekodi kutoka nchini Marekani. Ametunga na kutayarisha zaidi ya vibao 26 vilivyoshika nafasi ya kwanza tangu kuanza kazi yake ya muziki wa R&B, na ameshinda tuzo 11 za Grammy Awards.

Babyface
Edmonds mnamo Mei 2013
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaKenneth Brian Edmonds
Amezaliwa10 Aprili 1959 (1959-04-10) (umri 65)
Indianapolis, Indiana, U.S.
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi
Ala
  • Sauti
  • gitaa
  • kinanda
Miaka ya kazi1977–hadi sasa
StudioChi Sound, SOLAR, Epic, Arista, Mercury, Motown, Def Jam
Ameshirikiana naToni Braxton, Whitney Houston, The Deele, Az Yet, Manchild, TLC, After 7
Wavutibabyfacemusic.com

Maisha ya awali hariri

Edmonds alizaliwa mnamo tarehe 10 Aprili, 1959, mjini Indianapolis, Indiana,[3][4][5] na Marvin na Barbara Edmonds. Barbara alikuwa msimamizi wa uzalishaji katika kiwanda cha dawa. Edmonds, ambaye ni wa sita kati ya familia ya watoto sita wa kiume (ikiwa ni pamoja na wanachama wa baadaye wa kundi la After 7 bwana Melvin na Kevon Edmonds, ambaye baadaye akaja kuwa msanii wa kujitegemea mwenye mafanikio makubwa sana). Edmonds alihitimu North Central High School huko mjini Indianapolis. Akiwa kijana mwenye aibu, alitunga wimbo wa kuelezea hisia zake.[6] Akiwa darasa la nane, baba mzazi wa Edmonds alifariki kwa kansa ya mapafu. Akamwacha mama yake akilea watoto peke yake.[6] Katika umri huu, Edmonds ankatazamia sasa kubaki na kazi ya muziki pekee.[3]

Kazi ya muziki hariri

Edmonds baadaye alicharaza na waimbaji wa funk kina Bootsy Collins, ambao walimpa jina la "Babyface" kutokana na mwonekanano wake wa kitoto. Vilevile aliwahi kufanya kazi na kundi la Manchild (ambalo lilitoa wimbo wake maarufu mnamo 1977 uliokwenda kwa jina la "Especially for You" akiwa na mwanachama Daryl Simmons) kama mpiga gitaa. Halkadhalika amewahi kucharaza kinanda na kundi la funk na R&B nyepesi na kundi la the Deele (ambalo pia lina mwanachama mwengine mpiga drama Antonio "L.A." Reid, ambaye baadaye akaja kuungana nae kwa kazi ya utunzi na utayarishaji wa kazi za muziki). Kazi yake ya kwanza kusifika ya kutungia wasanii wa nje mbali na wale wa kundi moja ilikuwa ya tuni ya "Slow Jam" kwa ajili ya bendi ya R&B ya Midnight Star mnamo mwaka wa 1983. Tuni hiyo imo kwenye albamu ya mwaka wa 1983 ya kundi la Midnight Star iliyogonga platinamu dabali No Parking on the Dance Floor, ajabu iliyoje haikuwa kama singo na lakini ilipokelewa vyema kabisa katika maredio mbalimbali. Babyface alibaki katika kundi la Deele hadi 1988, ambapo wote wawili yeye na Reid alivyoliacha kundi.

Albamu yake ya Playlist ina nyimbo nane za kurudia kutoka kwa wasanii wengine na mbili nyimbo zake. Ilitolewa mnamo tarere 18 Septemba, 2007. Hii ndio albamu ya kwanza kutolewa upya na lebo ya Mercury Records label.[7]

 
Edmonds akitumbuiza mnamo mwaka wa 2009

Mnamo tarehe 4 Februari, 2014, alitoa albamu iliyoshinda tuzo za Grammy Award akiwa na Toni Braxton iliyokwenda kwa jina la Love, Marriage & Divorce kupitia Motown Records.[8]

Kazi nyengine hariri

Kigezo:BLP sources section

Kutunga na kutayarisha hariri

Mwishoni mwa miaka ya 1980, alichangia kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa new jack swing, alitunga na kutayarisha muziki kwa ajili ya wasanii kama kina Bobby Brown, Karyn White, Pebbles, Paula Abdul, Michael Jackson na Sheena Easton.

Mwaka wa 1989, Edmonds alikuwa mmoja wa waanzilishi wa studio ya LaFace Records akiwa na Reid. Wasanii watatu wa kwanza katika lebo hii ni pamoja na TLC, Usher, na Toni Braxton ambao walipata mafanikio makubwa sana. Albamu ya pili ya TLC CrazySexyCool, alitunga na kutayarisha baadhi ya vibao vikali kutoka katika albamu hiyo. Baadaye ikaja kuwa moja kati ya albamu iliyouza sana kwa upande wa makundi ya muziki ya wasichana nchini Marekani. Chini ya uongozi wake, TLC waliweza kuuza nakala zaidi ya milioni 60 duniani kote, na kujumuisha jumla ya rekodi milioni 75 kwa kazi zote walizofanya nae. Albamu ya kwanza ya Toni Braxton, Toni Braxton (1993) na Secrets (1996), ambayo ametunga sehemu kubwa ya nyimbo, ilikwenda kuuza jumla ya nakala milioni kwa Marekani pekee.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, Babyface alisadia kundwa kwa kundi la muziki wa R&B—Az Yet. Halkadhali Edmonds alisaidia kumjenga na kufanya kazi na wasanii wa mkewe wa zamani Bi. Tracey Edmonds, kama vile Jon B mtayarishaji Jon-John Robinson.

Edmonds amefanya kazi na wasanii wengi sana wenye mafanikio katika muziki wa R&B. “I’m Your Baby Tonight” (1990), aliutayarisha kwa ajili ya Whitney Houston, kilikuwa kibao chake cha kwanza kushika Na. 1 kwenye Top 40 nchini Marekani. Vilevile alitunga na kutayarisha wimbo wa Boyz II Men wa mwaka wa 1992 "End of the Road" na 1994 "I'll Make Love to You", zote mbili ziliweza kudumu sana kwenye nafasi ya 1 kwenye chati za Billboard Hot 100. Alishiriki kutunga, kutayarisha, na kusaidia kuitikia katika albamu ya Madonna ya mwaka 1994 Bedtime Stories, ambayo ina kibao kilichoshika majuma saba kwenye chati cha "Take a Bow". Vilevile ametunga na kutayarisha kibao kilichoshika nafasi ya kwanza "Exhale (Shoop Shoop)" kwa ajili ya Whitney Houston halkadhalika vibao vingine vyote vilivyokuja kuuza nakala milioni 10 kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Waiting to Exhale mnamo mwaka wa 1995, ambayo ilitamba zaidi kwa vibao vya Houston, Brandy na Mary J. Blige.

Vilevile, Edmonds ametayarisha na kutunga vibao chungumzima kwa ajili ya wasanii kama vile Carole King, Patti LaBelle, Chaka Khan, Aretha Franklin, Madonna, Janet Jackson, Faith Evans, Al Green, Beyoncé, Diana Ross, Sheena Easton, Toni Braxton, Michael Jackson, Michael Bolton, Paula Abdul, Eric Clapton, Pebbles, Tevin Campbell, Bobby Brown, Whitney Houston, Brandy, Mary J. Blige, Tamia, Shola Ama, 3T, Sisqó, Dru Hill, Fall Out Boy, Céline Dion, Samantha Jade, Backstreet Boys, Honeyz, Katharine McPhee, Mariah Carey, Vanessa L. Williams, Bruno Mars, Kelly Clarkson, Chanté Moore, En Vogue, Zendaya, Kenny G, Kristinia DeBarge, Lil Wayne, Japanese singer Ken Hirai, P!nk, Colbie Caillat, Marc Nelson, TLC, Ariana Grande, Ella Henderson, Jessica Mauboy, Xscape, K-Ci & JoJo, NSYNC, Jordin Sparks na Phil Collins na wengine kibao. Amepata Tuzo za Grammy ya Mtayarishaji wa Mwaka mara tatu mfululizo tangu 1995 1997.

Maisha binafsi hariri

Babyface alimwoa mke wake wa kwanza, Denise akiwa katika umri wake wa ujana kabisa. Mwaka wa 1990, Babyface anakutana na Tracey Edmonds wakati wa kusailiwa kwa ajili ya video ya muziki wake yeye mwenyewe maarufu wa "Whip Appeal". Walikuja kuoana mnamo tarehe 5 Septemba, 1992, na walijaaliwa watoto wawili, Brandon na Dylan. Mnamo tarehe 7 Januari, 2005, Tracey alifungua jalada la talaka katika mahakama kuu huko mjini Los Angeles, kielezea tofauti zisizosuluhusisha. Mwezi wa Oktoba 2005, Babyface na Tracey walitengana—wanamaliza ndoa yao iliyodumu kwa muda wa miaka kumi na tatu.

Mwaka wa 2007, Babyface alianza kujihusisha mahusiano na mnenguaji wake msaidizi Bi. Nicole "Nikki" Pantenburg (alikuwa mnenguaji msaidizi na rafiki wa karibu sana na Janet Jackson). Mwaka wa 2008, Babyface alijipatia mtoto wa kike.[9] Wawili hawa walikuja kuoana mnamo tarehe 17 Mei, 2014.

Mwaka wa 2015, Babyface alichangia fedha za kampeni kwa ajili ya mgombea urais kupitia chama cha Republican Seneta Marco Rubio.[10]

Urithi hariri

Mwaka wa 1999, njia yenye km 40 huko Indianapolis ilibadilishwa jina na kuitwa "Babyface" Edmonds Highway.[11]

Discografia hariri

Albamu akiwa msanii wa kujitegemea
Albamu za ushirika

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. "Babyface - Biography". biography.com. A&E Television Networks, LLC. Iliwekwa mnamo 2015-04-15. 
  2. "Kenneth "Babyface" Edmonds - Topics". bet.com. Black Entertainment Television, LLC. Iliwekwa mnamo 2015-04-15. 
  3. 3.0 3.1 Simon Glickman and Kelly Winters. "Babyface Biography". musicianguide. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo June 12, 2011. Iliwekwa mnamo May 10, 2011.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  4. Steve Huey. "Babyface Biography". allmusic. Iliwekwa mnamo May 10, 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. Sing to Me: My Story of Making Music, Finding Magic, and Searching for Who's Next - L.A. Reid In page 54, he said "Kenny was twenty-four years old (in 1983) - three years younger than me" 9 780062 274755
  6. 6.0 6.1 "Babyface Biography". AskMen. Iliwekwa mnamo May 10, 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "Babyface official website on Island Records". Island Records. January 20, 2007. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-25. Iliwekwa mnamo February 3, 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  8. "Love, Marriage & Divorce – Babyface, Toni Braxton | Songs, Reviews, Credits, Awards". AllMusic. Iliwekwa mnamo February 3, 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. Wihlborg, Ulrica (September 26, 2008). "Kenneth 'Babyface' Edmonds Is a New Dad! – Babies, Kenneth \Babyface\ Edmonds". People.com. Iliwekwa mnamo February 3, 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  10. "OnPolitics - USA TODAY's politics blog". 
  11. "Babyface Biography". Perfect People. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo February 21, 2014. Iliwekwa mnamo February 3, 2014.  Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)

Viungo vya Nje hariri