Bahari ya Eire (kwa Kiingereza: Irish Sea) ni sehemu ya bahari inayotenganisha visiwa vya Eire (Ireland) na Britania.

Ramani ya Bahari ya Eire (Irish Sea).

Ndani yake kuna visiwa viwili vikubwa kiasi ambayo ni Anglesey (Welisi) na Isle of Man, pamoja na visiwa vidogo.

Inapakana na nchi za Welisi, Uingereza na Uskoti (zote sehemu za Ufalme wa Muungano) upande wa mashariki, halafu Eire na Eire ya Kaskazini (pia sehemu ya Ufalme wa Muungano) upande wa magharibi.

Kila mwaka kuna abiria milioni 12 wanaovuka bahari hii na bidhaa tani milioni 17 zinasafirishwa kati ya Britania na Eire.

Uchumi

hariri

Eneo lake ni kilomita za mraba 46,007. Kina kirefu kinafikia mita 300 lakini kwa wastani ni mnamo mita 50[1].

Uvuvi ni biashara muhimu, mwaka 2008 samaki tani 38,000 walikamatwa [2].

Chini ya bahari hii kuna akiba za mafuta na gesi pamoja na vituo vya kuchimba maliasili hizi[3].

Marejeo

hariri
  1. "Irish Sea facts". Irish Sea Conservation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-11. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2015. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. [1] Ilihifadhiwa 11 Mei 2011 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Irish Sea Conservation, ilingaliwa Septemba 2019
  3. "Ireland offshore oilfield has over 1bn barrels, says drilling company". Guardian News and Media Limited. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons