Bahari ya Scotia ni eneo la bahari kati ya Antaktiki na Amerika Kusini pale ambako Bahari ya Kusini na Atlantiki Kusini zinakutana. Eneo la Bahari ya Scotia ni takribani kilomita za mraba 900,000.

Eneo la bahari ya Scotia kati ya Amerika Kusini na Antaktiki.
Ramani ya Bahari ya Scotia.

Mipaka yake ni Mapito ya Drake upande wa magharibi na Pinde la Scotia upande wa mashariki ambalo ni safu ya milima chini ya uso wa bahari inayounganisha Rasi Antaktiki na Nchi ya Moto (Tierra del Fuego). Sehemu ya milima hii huonekana kama visiwa vya Falkland, vya South Georgia na South Sandwich.

Visiwa hivyo ni vya mawe na sehemu kufunikwa na barafu na theluji mwaka wote. Bahari ya Scotia ni sehemu baridi yenye dhoruba nyingi.

Jina limetokana kuanzia mwaka 1932 na meli "Scotia" iliyotumwa 1902-1904 kutoka Uskoti kwa madhumuni ya msafara wa kisayansi ili kupeleleza hali ya Antaktiki.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: