Bahari ya Kusini
Bahari ya Kusini (pia: Bahari ya Antaktiki) ni jina jipya katika jiografia. Linamaanisha maji yote ya kusini ya latitudo ya 60 yanayozunguka bara la Antaktiki.
Katika eneo hilo maji ya Bahari ya Atlantiki, Bahari Hindi na Pasifiki hukutana na kuingiliana. Kwa muda mrefu wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Hidrografia walihesabu eneo kama vitengo vya kusini vya bahari hizo tatu kubwa lakini katika karne ya 20 wazo la kuitazama kama bahari ya pekee imesambaa na Bahari ya Kusini imerudi kwenye ramani. [1]
Eneo lote ni la kilomita za mraba 20,327,000 za maji. Linazunguka pwani ya Antaktiki yenye urefu wa kilomita 17,968. Kina kirefu ni mita 5,805 hivi.
Sehemu zake karibu na pwani hufunikwa na barafu inayokua wakati wa baridi. Katika miezi ya joto vipande vikubwa vya barafu humeguka na kuelea katika maji kama siwa barafu ambayo ni hatari kwa meli lakini zinayeyuka polepole kadiri zinavyofikia maji yasiyo baridi.
Marejeo
hariri- ↑ Taarifa ya IHO ya 1937 Ilihifadhiwa 8 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine. ilifuta jina la Bahari ya Kusini, lakini katika nakala ya 2002, mlango wa 10 Ilihifadhiwa 2 Februari 2014 kwenye Wayback Machine. imerudishwa.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|