Bamba la Australia
Bamba la Australia ni moja kati ya mabamba ya gandunia makubwa kwenye ganda la dunia. Wakati mwingine linahesabiwa pamoja na bamba la Uhindi kama "bamba la Australia-Uhindi".
Linabeba bara la Australia, kisiwa cha Guinea Mpya na sehemu za New Zealand, upande wa mashariki wa Bahari Hindi na sehemu ya Bahari Pasifiki.
Bamba la Australia limepakana na bamba la Ulaya-Asia, Bamba la Ufilipino, Bamba la Pasifiki, bamba la Antaktika na bamba la Afrika.