Baudeli (pia: Baudile, Bausile, Basile, Baudilio, Baudelio, Boal, Boi, Baldiri; alifariki Nimes, Ufaransa wa leo) ni kati ya Wakristo waliouawa[1] kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi yao[2].

Mt. Baudeli katika dirisha la Kanisa kuu la Nimes.

Ingawa hakuwa wa kwanza kuinjilisha eneo hilo la Galia, ndiye anayesifiwa zaidi kwa hilo. Inasemekana alikuwa shemasi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Mei[4]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.