Kisiwa cha Bawe

(Elekezwa kutoka Bawe island)

Kisiwa cha Bawe ni kisiwa kidogo kimojawapo cha funguvisiwa la Zanzibar (Tanzania) ambacho kinapatikana katika Bahari ya Hindi. Kipo takriban kilomita 10 (maili 6.2) baharini kutoka Stone Town, mji mkuu wa Zanzibar kwenye kisiwa cha Unguja.

Hakina wakazi ila kinatembelewa na watalii kikiwa chini ya Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi[1].

Historia

hariri

Mwishoni mwa karne ya 18, sultani Barghash ibn Sa'id wa Zanzibar alikitoa kisiwa hicho kwa kampuni ya Eastern Telegraph, ambayo ilikitumia kama kituo cha uendeshaji wa waya wa chini ya bahari unaounganisha Zanzibar na Shelisheli na Aden. Mkataba huo uliongezewa muda na sultani Khalifa ibn Said mwaka 1889, kwa faida ya kampuni ya Cable & Wireless, ambayo ilijenga nyumba kwenye kisiwa hicho kuwahudumia wafanyakazi wao. Leo hii, Bawe ni kivutio cha watalii pekee.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-10. Iliwekwa mnamo 2019-02-09.