Benki ya Wanawake Tanzania

Benki ya wanawake Tanzania (kwa Kiingereza: Tanzania Women Bank Limited; kifupi: TWBL) ni benki ya Tanzania ambayo ina utaalamu katika kutoa huduma za kifedha kwa wanawake. Imeorodheshwa kama "Taasisi ya Fedha iliyosajiliwa" na Benki Kuu ya Tanzania, mdhibiti wa benki za taifa.[1]

Benki hii ni taasisi ndogo ya kifedha nchini Tanzania, ambapo usawa wa wanahisa wa benki hiyo ulikuwa na thamani ya TSh8.5 bilioni (takriban dola milioni 4 za Kimarekani).[2]

Historia hariri

Wazo la kuanzisha Benki ya Wanawake nchini Tanzania lilianza mnamo mwaka 1999, wakati wajasiriamali kadhaa wa kike walipomwendea Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin William Mkapa, na wazo hilo. Baada ya miaka nane, mnamo mwaka 2007, Benki ya Wanawake Tanzania iliundwa. Benki ilifunguliwa rasmi kwa biashara mnamo Julai 28, mwaka 2009. Lengo la TWB ni kuwawezesha wanawake kiuchumi na kijamii. Benki hii inatumika kwa jamii zote ikiwa ni pamoja na wenye kipato cha chini, mashirika makubwa na biashara ndogo na za kati (SMEs).[3]

Mtandao wa matawi hariri

Mnamo Novemba mwaka 2014, benki hii ilikua na matawi katika maeneo yafuatayo:[4]

  1. Tawi la Mkwepu - Jengo la Posta ya Zamani, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam
  2. Tawi la Kariakoo - Mtaa wa Aggrey Likoma, Dar es Salaam
  3. Tawi la Dodoma - Jengo la Posta / TTCL, Barabara ya Reli, Dodoma
  4. Tawi la Mwanza - Jengo la Ofisi ya Zamani, Barabara ya Posta, Mwanza

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  1. BOT, . "Directory of Financial Institutions Operating in Tanzania". Bank of Tanzania (BOT). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-19. Iliwekwa mnamo 22 November 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. TDN (29 January 2016). "Tanzania: Women's Bank for Expansion". Tanzania Daily News (TDN) via AllAfrica.com. Dar es Salaam. Iliwekwa mnamo 31 January 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. TWB, . "Tanzania Women's Bank History". Tanzania Women's Bank (TWB). Iliwekwa mnamo 22 November 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. TWB, . "The Branches of Tanzania Women's Bank". Tanzania Women's Bank (TWB). Iliwekwa mnamo 22 November 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benki ya Wanawake Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.