Benjamin Mkapa

(Elekezwa kutoka Benjamin William Mkapa)

Benjamini William Mkapa (amezaliwa 12 Novemba 1938) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi, CCM (Revolutionary State Party).[1]

Benjamin Mkapa


Muda wa Utawala
23 November 1995 – 21 December 2005
Makamu wa Rais Omar Ali Juma (1995–2001)
Ali Mohamed Shein (2001-05)
mtangulizi Ali Hassan Mwinyi
aliyemfuata Jakaya Kikwete

Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu,
Muda wa Utawala
1992 – 1995
Rais Ali Hassan Mwinyi

Waziri wa Habari na Utangazaji
Muda wa Utawala
1990 – 1992
Rais Ali Hassan Mwinyi

tarehe ya kuzaliwa 12 Novemba 1938 (1938-11-12) (umri 81)
Ndanda, Masasi, Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama CCM
ndoa Anna Mkapa
watoto 2
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere
Chuo Kikuu cha Columbia
Fani yake mwandishi wa habari, mwanadiplomasia
dini Ukristo
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Ukoloni
Mgawanyo wa Afrika
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Uhuru
Mapinduzi ya Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
{Kigezo:Data99

Tanzania Portal

WasifuEdit

Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere.[1] Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.[2]

Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kuuungwa mkono kwa nguvu na rais wa zamani Julius Nyerere [3]. Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.[3]

Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha kampuni zilizomilikiwa na serikali akaweka sera za soko huria.[4] Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.[3]

Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi [3] vilevile matumizi mabaya ya fedha za umma. Utawala wake ulikuwa na matumizi sana na maposho bila kikomo. Alitumia £ 15 milioni kununua ndege ya binafsi ya kirais, vilevile karibu £ 30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalamu waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi.[5] Ilikuwa juu ya ununuzi huo wa mwisho ndipo Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.

Baada ya kutoka ofisini kwa kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa alikumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu.

Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.[4]

Heshima na TuzoEdit

NishaniEdit

Nishani Nchi Mwaka Ref
  Nishani ya Moyo wa Dhahabu wa Kenya (Chifu)   Kenya 2005 [6]
  Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere   Tanzania 2011

Mnamo Desemba 7, 2019, alitunukiwa Nishani ya Heshima ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake.

Shahada za HeshimaEdit

Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Mwaka Ref
Chuo Kikuu cha Sōka   Japan Shahada ya Heshima 1998 [7]
Chuo cha Morehouse   Marekani Shahada ya Heshima 1999 [7]
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania   Tanzania Shahada ya Heshima 2003 [7]
Chuo Kikuu ya Kitaifa cha Lesotho   Lesotho Daktari wa Sheria 2005 [7]
Chuo Kikuu cha Kenyatta   Kenya Daktari wa Elimu 2005 [8]
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam   Tanzania Shahada ya Heshima 2005 [7]
Chuo Kikuu cha Nyukasal   Uingereza Daktari wa Sheria ya Kiraia 2007 [9]
Chuo Kikuu cha Rasi ya Pwani (Cape Coast)   Ghana Daktari wa Barua 2008 [10]
Chuo Kikuu cha Makerere
  Uganda Daktari wa Sheria 2009 [11]

MarejeoEdit

 1. 1.0 1.1 "Benjamin Mkapa", Microsoft Encarta Encyclopedia 2001, WGBH (FM), pbs.org, ilitolewa 19-Oktoba-2009
 2. Benjamin Mkapa,
 3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Bruce Heilman na Laurean Ndumbaro, "Corruption, Politics and Societal Values in Tanzania: An Evaluation of the Mkapa Administration's Anti-Corruption Efforts", Afr. J. polit. sd. (2002), Toleo 1 Nambari 7
 4. 4.0 4.1 "Mheshimiwa Benjamin William Mkapa", Bodi ya Wadhamini, Chuo cha AKU, ilitolewa 19-10-2009
 5. Gideoni Burrows, "We sell arms to Saddam's friends", New Statesman, 8 Septemba 2003
 6. Mkapa lauds Kenya's democratic posture. panapress.com (12 October 2005). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
 7. 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 83RD Annual District Conference & Assembly (PDF) (Kiingereza). Page 10, Rotary International District 9200 (17 May 2008). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
 8. Prominent Alumni (Kiingereza). Kenyatta University. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
 9. Citation: Benjamin William Mkapa DCL (PDF) (Kiingereza). Newcastle University (2007). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
 10. UCC honours former Tanzanian leader (Kiingereza). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
 11. H.E. Benjamin Mkapa receives Makerere Honorary PhD (Kiingereza). Makerere University (27 November 2009). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.

Viungo vya njeEdit

Alitanguliwa na
Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Tanzania
1995-2005
Akafuatiwa na
Jakaya Kikwete

Viungo vya njeEdit

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: