Moma
Moma | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Moma wa kawaida au bafe
Bitis arietans | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 18:
|
Moma ni spishi za nyoka wenye sumu wa jenasi Bitis katika familia Viperidae. Spishi moja huitwa bafe pia na spishi nyingine wa familia Viperidae huitwa vipiri.
Spishi nyingi za moma, zile za Afrika ya Mashariki hasa, ni kubwa na nene kuliko vipiri wengine, lakini spishi kadhaa ni ndogo zaidi na moma mdogo wa Namakwa ni mdogo kabisa wa Viperidae wote duniani. Kinyume chake moma-misitu ni mkubwa kabisa.
Wakitishwa moma hutuna na kujipojaa wakifyonya kwa sauti kubwa. Inaonekana kama sio wepesi lakini wanaweza kupiga kwa kasi ya umeme.
Nyoka hawa ni wanene na wazito kwa kulinganisha na urefu wao. Wana kichwa kipana kwa umbo wa pembetatu na mkia mfupi. Magamba yao yana miinuko na yale ya pua yanaweza kuwa marefu na kufanana na pembe.
Spishi
hariri- Bitis albanica, Moma wa Albany (Albany adder)
- Bitis arietans, Bafe au Moma wa Kawaida (African puff adder)
- Bitis armata, Moma Kusi (Southern adder)
- Bitis atropos, Moma-milima Kusi (Mountain adder)
- Bitis caudalis, Moma Pembe (Horned adder)
- Bitis cornuta, Moma Pembe-nyingi (Many-horned adder)
- Bitis gabonica, Moma- au Kifutu-misitu (Gaboon viper)
- Bitis harenna, Moma wa Dodola (Dodola adder)
- Bitis heraldica, Moma wa Angola (Angolan adder)
- Bitis inornata, Moma Mfuto (Plain mountain adder)
- Bitis nasicornis, Moma-milima au Kifutu-milima (Rhinoceros viper)
- Bitis parviocula, Moma wa Bale (Bale Mountains adder)
- Bitis peringueyi, Moma Mdogo (Dwarf puff adder)
- Bitis rhinoceros, Moma Kifaru (Rhinoceros adder)
- Bitis rubida, Moma Mwekundu (Red adder)
- Bitis schneideri, Moma Mdogo wa Namakwa (Namaqua puff adder)
- Bitis worthingtoni, Moma wa Kenya au Kifutu-pembe wa Kenya (Kenya horned viper)
- Bitis xeropaga, Moma-njangwa (Desert mountain adder)
Picha
hariri-
Moma-milima kusi
-
Moma pembe
-
Moma pembe-nyingi
-
Moma-misitu
-
Moma-milima
-
Moma wa Bale
-
Moma mdogo
-
Moma kifaru
-
Moma mwekundu
-
Moma mdogo wa Namakwa
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Moma kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |