Ludwig van Beethoven

Ludwig van Beethoven (16 Desemba 1770 - 26 Machi 1827) alikuwa mtungaji wa muziki na mpiga piano kutoka nchi ya Ujerumani.

Ludwig van Beethoven (1770–1827) alivyochorwa na Joseph Karl Stieler, 1820.
Picha yake katika stempu ya Ujerumani ya mwaka 1970.

MaishaEdit

Alizaliwa mjini Bonn akiwa mtoto wa mwanamuziki aliyemfundisha kupiga kinanda tangu utotoni.

Mwaka 1787 akiwa kijana alisafiri hadi Vienna uliokuwa mji mkuu wa Dola Takatifu la Kiroma kwa matumaini ya kukutana na Wolfgang Amadeus Mozart akarudi huko mwaka 1792 alipopata mafunzo kutoka kwa Joseph Haydn.

Tangu mwaka 1793 alikuwa maarufu mjini Vienna kama mpigakinanda akaendelea kutunga muziki wake. Alipata msaada wa wateja kati ya makabaila wa makao makuu ya Kaisari.

Tangu mwaka 1796 alianza kupoteza uwezo wake wa kusikia akazidi kuwa kiziwi lakini aliamua kuendelea na muziki wake. Kuna hadithi ya kwamba aliongoza simfonia ya tisa na mwishowe watu walimgeuza aangalie wasikilizaji kwa sababu hakusikia jinsi walivyopiga makofi.

Alijitahidi kuendelea kutunga na kuongoza muziki na kupiga piano. Alifunga fimbo kwenye kinanda akaishika kwa meno na kusikia walau tetemeko la piano kupitia fimbo na meno yake.

Aliaga dunia alipokuwa na umri wa miaka 57.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Orodha ya Wanamuziki wa kipindi cha Romatiki
Alkan Balakirev Beethoven Bellini Berlioz Berwald Bizet Borodin Brahms Bruckner Chopin Cui Dvořák Elgar Field Franck Glinka Grieg Liszt Mahler Mendelssohn Mussorgsky Rachmaninoff Rimsky-Korsakov Saint-Saëns Schubert Schumann Smetana Strauss Tchaikovsky Verdi Wagner Wolf Weber

  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Ulaya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ludwig van Beethoven kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.