Köln

(Elekezwa kutoka Cologne)

Köln (pia: Kolon (kutokana na Kiing. Cologne; Kijerumani cha kienyeji: Kölle) ni mji wa Kijerumani kando la mto Rhine mwenye wakazi 970,000. Maana ya kiasili ya jina ni "koloni".

Köln

Bendera

Nembo
Köln is located in Ujerumani
Köln
Köln
Mahali pa mji wa Köln katika Ujerumani
Majiranukta: 50°56′0″N 6°57′0″E / 50.93333°N 6.95°E / 50.93333; 6.95
Nchi Ujerumani
Jimbo Rhine Kaskazini - Westfalia
Idadi ya wakazi (2009)
 - 998,105
Tovuti: www.koeln.de

Ni mji wa kale ulioundwa kwa jina la "Colonia Claudia Ara Agrippinensis" kama koloni ya Waroma wa Kale mnamo mwaka 50. Mahali pa mji paliwahi kuwa boma la Kiroma na kabla ya hayo kijiji cha kabila cha Waubii.

Köln ni mji mkubwa wa nne wa Ujerumani na mji mkubwa wa jimbo la Rhine Kaskazini - Westfalia (Nordrhein-Westfalen).

Kuna kanisa kubwa la Ujerumani wote ("Kölner Dom") ambalo ni maarufu kwa sababu limejengwa katika muda miaka 700 tangu mwaka 1248 hadi 1880. Masalio ya mamajusi watatu waliomtembelea mtoto Yesu huko Bethlehemu yanasemekana kutunzwa humo. Köln ni kitovu muhimu wa kanisa katoliki na makao wa askofu mkuu.

Chuo kikuu chake kilianzishwa mwaka 1388 na leo kuna wanafunzi 44,000 na pamoja na vyuo vingine kuna wanafunzi zaidi ya 80,000 kwenye ngazi ya vyuo. Kati ya vyuo vingini Chuo cha Muziki kimejulikana sana kimataifa.

Mji umejulikana nchini kwa aina yake ya pekee ya bia.

Köln ni pia kitovu cha Waafrika katika Ujerumani. Pamoja na wanafunzi wengi kutoka Afrika kuna pia taasisi kama huduma ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) zinazoajiri Waafrika wengi. Kuna hata vilabu ambako bia aina ya Tusker kutoka Kenya inauzwa.

Mwaka 2005 Köln ilikuwa mahali pa mkutano wa Vijana Wakatoliki Duniani wakakutana zaidi ya milioni moja na Papa Benedikto XVI.

Watalii wengi wanakuja kila mwaka kwa sherehe ya Karnivali kabla ya majira ya kwaresima.

Tazama piaEdit

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Köln kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.