Milki ya Bornu
Bornu (pia Borno[1]) ilikuwa milki muhimu katika Afrika ya Magharibi kwenye ukanda wa Saheli katika maeneo ya nchi za leo Nigeria, Niger na Chadi.
Mnamo mwaka 1800 ilikuwa na uenezaji mkubwa na kumiliki eneo la takriban kilomita za mraba 242.701 pamoja na Ziwa Chad. Ilipakana wakati ule na Mandara, Emirati ya Adamawa, Ukhalifa wa Sokoto na maeneo ya Watuareg kwenye Sahara.
Bornu ilivamiwa mwaka 1893 na mfanyabiashara Mwarabu Rabih ben Fadlallah aliyeshinda na kuua watawala wake. Mwenyewe alivamiwa na Wafaransa waliopanua himaya yao barani Afrika wakati ule. Milki ya Bornu iligawiwa kati ya Ufaransa, Uingereza na Ujerumani.
Sehemu ya Kiingereza iliingizwa katika koloni la Nigeria na hapo kuendelea kwa jina kama milki chini ya "shehu" wa familia ya wafalme wa kale lakini chini ya usimamizi wa Waingereza. Milki hii inaendelea kwa jina katika jimbo la Nigeria linaloitwa Borno.
Viungo vya nje
haririTanbihi
hariri- ↑ Katika Wikipedia hii tunatumia "Bornu" kama jina la milki ya kihistoria na "Borno" kama jina la jimbo la Nigeria ingawa ni neno lilelile
Kujisomea
hariri- Brenner, Louis: The Shehus of Kukawa, Oxford 1973.
- Cohen, Ronald: The Kanuri of Bornu, New York 1967.
- Hughes, William (2007). A class-book of modern geography (Paperback). Whitefish, MT: Kessinger Publishing. uk. 390 Pages. ISBN 1-4326-8180-X.
- Lange, Dierk: Le Dīwān des sultans du Kanem-Bornu, Wiesbaden 1977.
- -- A Sudanic Chronicle: The Borno Expeditions of Idris Alauma (1564-1576), Stuttgart 1987.
- -- "Ethnogenesis from within the Chadic state", Paideuma, 39 (1993), 261-277.
- Nachtigal, Gustav: Sahara und Sudan, Berlin, 1879-1881, Leipzig 1989 (Nachdruck Graz 1967; engl. Übers. von Humphrey Fisher).
- Oliver, Roland & Anthony Atmore (2005). Africa Since 1800, Fifth Edition. Cambridge: Cambridge University Press. uk. 405 Pages. ISBN 0-521-83615-8.
- Urvoy, Yves: L'empire du Bornou, Paris 1949.
- Zakari, Maikorema: Contribution à l'histoire des populations du sud-est nigérien, Niamey 1985.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Milki ya Bornu kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |