Bosha
Bosha ni moja ya kata zilizopo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,754 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,585 [2] waishio humo.
Kabila kubwa la wakazi wa kata ya Bosha ni Wasambaa ingawa kuna mchanganyiko wa Wazigua, Wabondei na makabila mengine.
Kata ya Bosha imezungukwa na milima ya Usambara pande zote nne.
Kata hii ina vijiji vilivyosajiliwa kiserikali vinne ambavyo ni Bosha Kwemtindi, Kuze Kibago, Muzi Kafishe, na Kwamtili.
Kata ya Bosha ina shule za msingi za serikali 7 ambazo ni Bosha, Kuze, Kwamtili, Kwemtindi, Muzi, Vumbu na Kibago.
Upande wa huduma za afya Bosha ina zahanati moja inayopatikana kijiji cha Kuze Kibago, ingawa kwa sasa serikali, kupitia halmashauri ya wilaya ya Mkinga inajenga zahanati nyingine 3 katika vijiji vya Muzi, Bosha (makao makuu ya kata) na Kwemtindi.
Asilimia 90 ya wakazi wa kata ya Bosha hutumia kilimo kama njia ya kujiendeleza kiuchumi na kupata chakula. Ufugaji wa nyuki kwenye misitu ya hifadhi ya Nilo na mifugo mingine ya nyumbani pia inasaidia kuinua uchumi wa wakazi.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Tanga - Mkinga DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
Kata za Wilaya ya Mkinga - Mkoa wa Tanga - Tanzania |
||
---|---|---|
Boma | Bosha | Bwiti | Daluni | Doda | Duga | Gombero | Kigongoi Magharibi | Kigongoi Mashariki | Kwale | Manza | Mapatano | Maramba | Mayomboni | Mhinduro | Mkinga | Mnyenzani | Moa | Mtimbwani | Mwakijembe | Parungu Kasera | Sigaya |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bosha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |