Mifugo au Wanyama wa kufugwa ni wanyama wanaopatikana kutokana na ufugaji wa kibinadamu.

Mchungaji na mifugo yake
Mifugo aina ya ng'ombe

Wako tofauti na wanyamapori baada ya na mchakato mrefu ambako wanyama wa pori ama walijiunga na binadamu au walishikwa nao na watoto wao kuteuliwa kutokana na tabia zilizopendelewa na wafugaji wao. Tabia hizo ni pamoja na upole na uwezo wa kupatana na binadamu, uwezo wa kuzalisha kiasi fulani cha nyama au maziwa, uwezo wa kustawi kwa chakula fulani au katika mazingira mbalimbali.

Katika mchakato wa vizazi vingi tabia zilizolengwa ziliimarishwa katika spishi zinazofugwa.

Uteuzi huu umesababisha tofauti za kimaumbile na tofauti za tabia baina ya wanyama wa kufugwa na wanyamapori wa spishi ileile. Tofauti hizi zinaonekana katika rangi, ukubwa wa mwili, uwezo wa kuwasiliana na binadamu na mengine.

Asili katika wanyama waliotafuta mazingira ya kibinadamu hariri

Imethibitishwa ya kwamba mnyama wa kwanza wa kufugwa alikuwa mbwa. Asili ya mbwa walikuwa vikundi vya mbwa mwitu wa Ulaya (wolf) waliofuata koo za binadamu wawindaji na kula mabaki ya chakula yaliyotupwa nao. Kwa kupatana na mbwa mwitu ambao walikuwa wapole na kutoshambulia watu (pamoja na kuua wote waliokuwa wakali) binadamu hao walianza kupatana nao na kuona faida ya uangalifu wao wakati mgeni au windo alikaribia. Tangu kuwapatia mbwa mwitu chakula kama zawadi waliendelea kuzoeana. Ingawa historia hii bado haieleweki kikamilifu, watalaamu wengine wanaona ya kwamba wawindaji kadhaa walianza kutunza watoto wa mbwa mwitu kwao na kuwafuga kama wanyama wapenzi.

Inaonekana ya kwamba kulikuwa pia na wanyama wengine wa porini waliofuata binadamu kwa sababu waliona faida kukaa karibu nao kama vile paka (aliyefuata panya waliokula mavuno ya wakulima wa kwanza).

Vilevile asili ya kuku ni kuku mwekundu wa porini wa Indonesia (red junglefowl) aliyetafuta takataka kwenye makazi ya watu, akawazoea na kutumiwa nao kama chanzo cha nyama na mayai.

Wanyama wa windo waliotunzwa na binadamu hariri

Wanyama walioteuliwa baadaye kwa ufugaji hariri

Tanbihi hariri


Marejeo hariri

  • [www.palaeobarn.com/sites/domestication.org.uk/files/downloads/112.pdf Larson, Fuller:The Evolution of Animal Domestication]