Bosporus

(Elekezwa kutoka Bosphorus)

Bosporus (Kituruki: Bogaziçi) ni mlango wa bahari katika Uturuki unaounganisha Bahari Nyeusi na Bahari ya Marmara. Mlango huu una urefu wa 32 km na sehemu nyembamba ni 640 m. Kina cha maji hufikia 36–124 m.

Bosporus kutoka angani (Bahari nyeusi iko juu; rangi nyekundu ni mji wa Istanbul
Bosporus kutoka angani
(Bahari nyeusi iko juu; rangi nyekundu ni mji wa Istanbul
Mahali pa Borporus
Bosporus, Istanbul

Mji wa Istanbul uko kwenye mwanzo wa Bosporus upande wa Bahari ya Marmara.

Kuna madaraja mawili ya kuvuka maji:

  • daraja la Bogaziçi limejengwa 1973 kwa urefu wa 1074 m.
  • daraja la Fatih Sultan Mehmed limejengwa 1988 kwa urefu wa 1090 m.

Ujenzi wa handaki ya reli chini ya bahari ulianza mwaka 2005.

Tangu 1936 mkataba wa Montreux umetawala haki za matumizi kwa meli za mataifa yote katika Borporus. Nchi zinazopakana na baharii nyeusi zinategemea njia hiyo kama vile Urusi, Ukraine, Bulgaria na Romania.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bosporus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.