Busambara
Busambara ni kata ya Wilaya ya Musoma Vijijini katika Mkoa wa Mara, Tanzania.
Kata ya Busambara inajumuisha vijiji vitatu ambavyo ni Kwikuba, Mwiringo na Maneke. Makao makuu ya kata ni kijiji cha Kwikuba.
Kata hii iko umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa Musoma, barabara kuu ya Majita Busekela.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,127 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,706 waishio humo.[2]
Wenyeji wa kata hii ni wa kabila la Waruri ingawa pia kuna makabila kama Wajita, Wakwaya, Wazanaki, Wakabwa, Wakurya, Wasukuma na Wajaluo.
Marejeo
haririKata za Musoma Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania |
||
---|---|---|
Bugoji | Bugwema | Bukima | Bukumi | Bulinga | Busambara | Bwasi | Etaro | Ifulifu | Kiriba | Makojo | Mugango | Murangi | Musanja | Nyakatende | Nyambono | Nyamrandirira | Nyegina | Rusoli | Suguti | Tegeruka |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Busambara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |