Ibrahim Haruna Lipumba (amezaliwa tar. 6 Juni 1952, Ilolangulu, Tabora, Tanzania) ni mwanasiasa nchini Tanzania na pia mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi)

Lipumba
Viongozi wa chama cha CUF Ndugu Seif Shariff Hamad (kushoto) na Prof. Lipumba (kulia)

Maisha ya Mwanzo na Elimu

hariri

Mh. Lipumba alizaliwa tar. 6 Juni Mwaka 1952, katika kiji cha Ilolangulu Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora Tanzania. Ameanza elimu ya msingi 1959 - 1962 katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 1962 - 1966 : L.A Upper Primary School, Sikonge

baadae kuendelea masomo na Elimu ya Sekondari 1967 hadi1970 Tabora Boys Secondary School 1971 hadi 1972 Pugu Secondary School Kisha Elimu ya Chuo Kikuu 1973 hadi 1977 University of Dar es Salaam 1978 hadi 1983 Stanford University. Akapata Shahada BA (Hon.Economics) University of Dar es Salaam 1976 MA (Economics) University of Dar es Salaam 1977 MA (Economics) Stanford University 1979 Phd (Economics) Stanford University1983

Uzoefu wa Uongozi

hariri

Aliwahi kuwa mweka hazina wa Umoja wa Vijana Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970 pia akawahi kuwa Katibu mkuwa wa Kikundi cha Majadiliano cha Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970, baadae akaja kuwa Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Vijana katika shule ya pugu Secondary School hiyo ilikuwa mwaka 1970 hadi 1971, baadae akaja kuwa tena Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka mwaka 1975 hadi 1976. na pia ndiye Mwanzilishi na Rais wa Kwanza wa Stanford African Students Association (SASA), Stanford University; Stanford, California USA hiyo ilikuwa mwaka 1978.

  • 1976 hadi 1977 Mkufunzi Msaidizi (T.A)
  • 1977 hadi 1983 Mhadhiri Msaidizi
  • 1983 hadi 1986 Mhadhiri
  • 1986 hadi 1989 Mhadhiri Mwandamizi
  • 1989 hadi 1993 Profesa Mshiriki
  • 1991 hadi 1993 Msaidizi wa Rais Mambo ya Uchumi
  • 1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professor, Williams College, Massachussets, United States of America
  • 1996 hadi 1998 Senior Research Fellow, United Nations University, World Institute of

Economic Research, Helsinki Finland.

Heshima za Kitaaluma

hariri
  • 1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professorship
  • 1986 hadi 1989 Kellogg International Fellow in Food Systems
  • 1977 hadi 1983 Rockefeller Foundation Fellowship
  • 1976 Zawadi ya Mwanafunzi Bora, Best Student

Award, Faculty of Arts and Social Sciences,University of Dar es Salaam.

Mshauri wa Uchumi

hariri

Shughuli za Kimataifa

hariri
 
Lipumba akiwa kwenye shughuli za Kimataifa

Utafiti kuhusu kushiriki kwa nchi za kusini katika mfumo wa biashara wa kimataifa, Uruguay Round Multilateral trade negotiations kuanzia mwaka 1986 ha 1990. Utafiti kuhusu sera za kilimo za nchi zinazoendelea. Kuwasilisha maelezo (Testmony) kuhusu matatizo ya madeni ya Afrika kwenye kamati ya Bunge la Marekani - House Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Februari 1994.

Kuwasilisha, maelezo (Testmony) kuhusu shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na uhusiano wake na nchi masikini kwenye kamati ya Bunge la Marekani House - Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Aprili 1994

Kutayarisha “Report of Group of Independent Advisers on Development Cooperation issues between Tanzania and Aid Donors”. Juni 1995

Kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya sera ya maendeleo (member of the United Nations Committee for Development Policy (1995 hadi 1999.)

Kutayarisha vigezo vya kuainisha nchi masikini sana duniani. (The list of Least Developed Countries (1997 na 2000)

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998).

Kutathmini maendeleo ya ‘The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa’, (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998.

Shughuli za Kitaifa

hariri
  • Mjumbe - Kamati ya kurekebisha mashirika ya umma, 1992 - 1993
  • Mwenyekiti - Tume ya kuchunguza matatizo ya chama cha ushirika cha mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), 1992
  • Mwenyekiti - Tume ya Waziri wa Fedha ya kuchunguza matatizo ya Shirika la Bima (NIC) 1993

Baadhi ya Tafiti za Uchumi na Maandishi Muhimu

hariri
  • Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984
  • African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, Mei 1983. Published by Stanford African Students Association.
  • Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1. No. 1, Aprili 1982.

Ona Pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri