Capers Jones ni mtaalamu wa uhandisi katika uandishi wa programu za mifumo wa Marekani, na mara nyingi huhusishwa na mifumo ya ukadiriaji wa gharama katika nyanja tofautitofauti.

Alizaliwa huko St Petersburg, Florida, Marekani na kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Florida, akiwa amehitimu na kubobea katika lugha ya Kiingereza[1]. Baadaye alikua Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Capers Jones & Associates[2] na baadaye Mwanasayansi Mkuu Emeritus wa Utafiti wa Tija za Programu (SPR)[3].

Mnamo mwaka 2011, alianzisha kampuni ya Namcook Analytics LLC, ambapo yeye ni Makamu wa Rais na Afisa Mkuu wa Teknolojia (CTO)[4].

Aliunda biashara yake mwenyewe mnamo 1984, Utafiti wa Tija za Programu, baada ya kushikilia nyadhifa katika IBM[5] na ITT[6]. Lakini baada ya kustaafu kutoka kwenye Utafiti wa Tija za Programu 2000, Casper anabaki tu kuwa kama mshauri.

Yeye ni Mshauri Mashuhuri wa Muungano wa Ubora wa Programu ya teknolojia ya habari (CISQ)[7].

Marejeo hariri

  1. Department of English | Alumni Profile: T. Capers Jones. web.archive.org (2012-04-04). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-04-04. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
  2. "Capers Jones", Wikipedia (in English), 2022-11-22, retrieved 2022-11-25 
  3. SPR | Technology Modernization Firm (en-US). SPR. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
  4. Homepage (en-US). The Barn Burner NamCook Analytics. Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-10-06. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
  5. IBM - United States (en-US). www.ibm.com (2015-10-01). Iliwekwa mnamo 2022-11-25.
  6. SPR | Technology Modernization Firm (en-US). SPR. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
  7. SEI News | Carnegie Mellon SEI and OMG Announce the Launch of CISQ—The Consortium for IT Software Quality (www.it-cisq.org) (en). SEI News. Iliwekwa mnamo 2022-08-10.
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Capers Jones kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.