Kirukanjia
|
|
Uainishaji wa kisayansi
|
Himaya:
|
Animalia (Wanyama)
|
Faila:
|
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila:
|
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli:
|
Aves (Ndege)
|
Oda:
|
Caprimulgiformes (Ndege kama virukanjia)
|
Familia:
|
Caprimulgidae (Ndege walio na mnasaba na virukanjia)
|
Jenasi:
|
Antrostomus Bonaparte, 1838
Caprimulgus Linnaeus, 1758
Chordeiles Swainson, 1832
Eleothreptus G.R. Gray, 1840
Eurostopodus Gould, 1838
Hydropsalis >Wagler, 1832
Lurocalis Cassin, 1851
Lyncornis Gould, 1838
Macrodipteryx Swainson, 1837
Macropsalis P.L. Sclater, 1866
Nyctidromus Gould, 1838
Nyctiphrynus Bonaparte, 1857
Nyctiprogne Bonaparte, 1857
Phalaenoptilus Ridgway, 1880
Siphonorhis P.L. Sclater, 1861
Uropsalis W. Miller, 1915
Veles Bangs, 1918
|
|
Virukanjia au mbarawaji ni ndege wa familia Caprimulgidae. Spishi nyingine zina majina kama gawa, mpasuasanda, pwaju, upapasa na rushana. Rangi yao ni kahawia au kijivu na madoa na michirizi meupe. Kuwaona ni kugumu, kwa sababu huruka usiku. Kwa kawaida watu huisikia sauti yao tu, lakini huonekana mara nyingi kwenye mwanga wa taa za mbele za gari. Huendelea kukaa chini hadi ya wakati wa mwisho kabla ya kupuruka; hii ni asili ya jina lao. Hukamata wadudu wa usiku wakiruka, kama nondo na kumbikumbi, lakini spishi kadhaa hula ndege wadogo pia. Jike huyataga mayai mawili chini.
- Caprimulgus aegyptius, Kirukanjia wa Misri (Egyptian Nightjar)
- Caprimulgus batesi, Kirukanjia wa Bates (Bates's Nightjar)
- Caprimulgus clarus, Kirukanjia Mkia-mwembamba (Slender-tailed Nightjar)
- Caprimulgus climacurus, Kirukanjia Mkia-mrefu (Long-tailed Nightjar)
- Caprimulgus donaldsoni, Kirukanjia Mwekundu (Donaldson-Smith's Nightjar)
- Caprimulgus enarratus, Kirukanjia Mkufu (Collared Nightjar)
- Caprimulgus europaeus, Kirukanjia wa Ulaya (European Nightjar)
- Caprimulgus eximius, Kirukanjia Dhahabu (Golden Nightjar)
- Caprimulgus fossii, Kirukanjia Kijivucheusi (Square-tailed Nightjar)
- Caprimulgus fraenatus, Kirukanjia Kahawia au Upapasa (Sombre Nightjar)
- Caprimulgus inornatus, Kirukanjia Bilachoro (Plain Nightjar)
- Caprimulgus madagascariensis, Kirukanjia wa Madagaska (Madagascar Nightjar)
- Caprimulgus natalensis, Kirukanjia Mkia-mweupe (Swamp Nightjar)
- Caprimulgus nigriscapularis, Kirukanjia Mabega-meusi (Black-shouldered Nightjar)
- Caprimulgus nubicus, Kirukanjia Nubi (Nubian Nightjar)
- Caprimulgus pectoralis, Kirukanjia Shingo-madoa (Fiery-necked Nightjar)
- Caprimulgus poliocephalus, Kirukanjia-milima (Montane Nightjar)
- Caprimulgus prigoginei, Kirukanjia wa Itombwe (Itombwe Nightjar)
- Caprimulgus ruficollis, Kirukanjia Shingo-nyekundu (Red-necked Nightjar)
- Caprimulgus rufigena, Kirukanjia Shavu-jekundu (Rufous-cheeked Nightjar)
- Caprimulgus ruwenzorii, Kirukanjia wa Ruwenzori (Ruwenzori Nightjar)
- Caprimulgus solala, Kirukanjia wa Nechisar (Nechisar Nightjar)
- Caprimulgus stellatus, Kirukanjia Madoa-nyota (Star-spotted Nightjar)
- Caprimulgus tristigma, Kirukanjia Madoa (Freckled Nightjar)
- Macrodipteryx longipennis, Kirukanjia Manyoya-mawili au Rushana (Standard-winged Nightjar)
- Macrodipteryx vexillarius, Kirukanjia Kalamu-mbili au Rushana Bawa-mraba (Pennant-winged Nightjar)
- Veles binotatus, Kirukanjia Madoa-mawili (Brown Nightjar)
Spishi za mabara mengine
hariri
-
Chuck-will's-widow
-
Large-tailed nightjar
-
Puerto Rican nightjar
-
Whip-poor-will