Shoro (Locustellidae)

(Elekezwa kutoka Catriscus)
Shoro
Shoro mkia-mpana
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Locustellidae (Ndege walio na mnasaba na shoro)
Bonaparte, 1854
Ngazi za chini

Jenasi 11:

Shoro ni ndege wadogo wa familia Locustellidae. Spishi za familia Acrocephalidae zinaitwa shoro pia. Shoro wa Locustellidae wana mkia mrefu kuliko wale wa Acrocephalidae. Rangi zao ni sawa lakini spishi nyingi zina michirizi myeusi mizito. Takriban spishi zote zinatokea maeneo ya tropiki na nusutropiki ya Afrika na Asia; spishi chache zinatokea maeneo baridi ya Ulaya na Asia na hizi huhamia Afrika na kusi ya Asia wakati wa majira ya baridi. Ndege hawa hupatikana sehemu za manyasi na vichaka, pengine misituni. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na pengine vijiti. Jike huyataga mayai 2-6.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri