Chad (ziwa)
Ziwa Chad ni ziwa kubwa lisilo na njia ya kutoka lenye kina kidogo katika kanda la Sahel, kando ya jangwa kubwa la Sahara, kule ambako nchi za Chad, Kamerun, Niger na Nigeria zinapopakana, hivi kwamba eneo lake limegawanywa kati ya nchi hizi. Ziwa Chad lina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa watu milioni 68 katika nchi hizo nne.
| |
Mahali | Afrika ya Kati |
Nchi zinazopakana | Chad, Kamerun, Nigeria, Niger |
Eneo la maji | 1500 km² |
Kina cha chini | hadi 7 m |
Mito inayoingia | Chari, Komadugu, Logone |
Mito inayotoka | --- |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
240 m |
Miji mikubwa ufukoni | -- |
Beseni yake ni beseni kubwa kwenye bara la Afrika. Hata hivyo, eneo la uso wake limebadilika katika mwendo wa karne zilizopita kutegemeana na kiasi cha maji kilichopokea na kiwango cha uvukizaji na matumizi ya maji yake.
Ziwa Chad lilipungua kwa asilimia 98 baina ya miaka 1963 na 1998 lakini picha za satelaiti za ESA zimeonyesha ya kwamba limepanuka tena kiasi. [1]
MarejeoEdit
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chad (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |