Chatu
Chatu | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chatu kaskazi
Python sebae | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 10:
|
Chatu ni spishi za nyoka katika jenasi Python wa familia Pythonidae. Kwa sababu hawana sumu lazima waue mawindo yao kwa njia nyingine. Kwa hivyo huzongamea mwili wao kuzunguka kidari cha mawindo kisha kubana kwa nguvu ili kuzuia mawindo asipumue mpaka afe halafu hummeza mzima.
Kwa kawaida chatu ni miongoni mwa majoka makubwa ambayo upata mawindo yake kwa kuvizia au kutega katika njia wapitamo mawindo. Kwa kawaida chatu hukamata wanyama wadogo kiasi kama vile panya, sungura, kanga, mbwa, mbuzi na paa. Spishi kubwa kama chatu kaskazini zinaweza kumeza ndama wa wanyama wakubwa kama vile swala, nyumbu, pofu, kondoo na ng'ombe, na hata binadamu na watoto wake lakini kwa nadra tu. Kwa hivyo kiumbe huyu inaweza kuwa hatari kwa maisha ya viumbe hai wengine.
Chatu kulingana na maumbile yao wapo wa aina kuu mbili yaani wembamba na wanene. Chatu wembamba mara nyingi hupatikana hasa katika maeneo ya milimani na chatu wanene hupatikana na upendelea kuishi hasa katika maeneo ya bondeni.
Spishi za Afrika
- Python anchietae, Chatu wa Angola (Angolan python)
- Python natalensis, Chatu Kusi (Southern African rock python)
- Python regius, Chatu Mfalme (Ball au Royal python)
- Python sebae, Chatu Kaskazi (Norther African rock python)
Spishi za Asia
- Python bivittatus (Burmese python)
- Python breitensteini (Bornean python)
- Python brongersmai (Blood python)
- Python curtus (Sumatran blood python)
- Python kyaiktiyo (Myanmar short-tailed python)
- Python molurus (Indian python)
- Python reticulatus (Reticulated python) – siku hizi huainishwa katika jenasi Malayopython
- Python timoriensis (Lesser Sundas python) – siku hizi huainishwa katika jenasi Malayopython
Picha
-
Chatu wa Angola
-
Chatu kusi
-
Chatu mfalme
-
Burmese python
-
Bornean python
-
Blood python
-
Myanmar short-tailed python
-
Indian python
-
Reticulated python
-
Lesser Sundas python
Marejeo
- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chatu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |