Jamhuri ya China
Taiwan, rasmi kama Jamhuri ya Uchina (ROC), ni nchi ya kisiwa katika Asia ya Mashariki, kilicho katika Bahari ya Pasifiki, kinachotenganishwa na Mlango wa Taiwan kutoka Jamuhuri y watu wa China. Inapakana na Uchina magharibi, Ufilipino kusini, na Japani kaskazini-mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 23.5, ikiwa ya 57 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni New Taipei, wakati mji mkuu ni Taipei. Taiwan imegawanyika katika mikoa 22, ikijumuisha miji mikuu maalum.
Jamhuri ya China 中華民國 | |
---|---|
Kaulimbiu: "三民主義,吾黨所宗" (Kichina kwa "Kanuni Tatu za Watu ni Msingi wa Chama Chetu") | |
Wimbo wa taifa: "中華民國國歌" (Zhōnghuá Mínguó Guógē) | |
Mji mkuu | Taipei |
Mji mkubwa | New Taipei |
Lugha rasmi | Kichina cha Mandarin |
Kabila (2020) | 95% Wahan 2.3% Wamataifa Asilia wa Taiwan |
Serikali | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kikatiba |
• Rais | Tsai Ing-wen |
• Waziri Mkuu | Chen Chien-jen |
Kujitenga na China Bara (de facto) | |
• Kuanguka kwa Dola ya Qing | 10 Oktoba 1911 |
• Kuanzishwa kwa Jamhuri ya China | 1 Januari 1912 |
• Serikali ya Jamhuri ya China kuhamia Taiwan | 7 Desemba 1949 |
Eneo | |
• Jumla | km2 36,193 (ya ya 137) |
• Maji (asilimia) | 8.6% |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2024 | 23,357,056 |
• Msongamano | 646/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $1.69 trilioni [1] (ya 21) |
• Kwa kila mtu | ▲ $71,373 [1](ya ) |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $829 bilioni [1] |
• Kwa kila mtu | ▲ $34,981 [1] |
HDI (2022) | 0.926 |
Sarafu | Dola Mpya ya Taiwan (NT$) TWD |
Majira ya saa | UTC+8 CST |
Upande wa magari | Kulia |
Msimbo wa simu | +886 |
Jina la kikoa | .tw |
Eneo
haririSehemu kubwa ya eneo lililo chini ya serikali ya Jamhuri ya China ni kisiwa cha Taiwan, lakini pia lina visiwa vidogo mbele ya mwambao wa China bara.
Mbali ya visiwa mbalimbali katika Bahari ya China visivyo na wakazi, upande wa magharibi kuna mafunguvisiwa matatu:
- Visiwa vya Wavuvi ama Pescadores - (Penghu, 澎湖列島)
- Quemoy (Kinmen, 金門)
- Matsu (馬祖列島)
Historia
haririJamhuri ya China iliundwa mwaka 1912 mjini Nanking baada ya mapinduzi ya China ya 1911 iliyomaliza utawala wa kifalme wa nasaba ya Qing. Sun Yat-sen akawa rais wa kwanza.
Serikali ya jamhuri ilidai mamlaka juu ya China yote ingawa hali halisi viongozi wa kijeshi na wapinzani mbalimbali walishika utawala katika maeneo kadhaa.
Nchi jinsi ilivyo sasa ni tokeo la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China iliyokwisha mwaka 1949 na ushindi wa Wakomunisti chini ya Mao Zedong na kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China huko Beijing.
Wakomunisti walifukuza serikali ya chama cha Kuomintang iliyoongoza Jamhuri ya China.
Mwaka 1949 serikali ya Kuomintang chini ya jenerali Chiang Kai-shek na mabaki ya jeshi lake pamoja na wafuasi wengi ilihamia Taiwan walipoendelea kutawala. Wakomunisti walikosa nguvu ya kuwafuata hadi kwenye visiwa kutokana na vitisho vya Marekani.
Hivyo serikali katika Taiwan iliendelea kujiita "serikali ya China" na kutangaza shabaha yake kuwa ukombozi wa China yote.
Hali halisi utawala wa Wakomunisti barani uliimarika na mipango yote kinyume chake ilionekana kama ndoto. Lakini kwa miaka minghi serikali ya Taipeh ilichukua nafasi ya China yote kimataifa.
Jamhuri ya China ilikuwa kati ya nchi zilizoanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 na serikali ya Kuomintang iliendelea kushika kiti cha China hadi mwaka 1971.
Tarehe 25 Oktoba 1971 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua ya kuwa Jamhuri ya Watu wa China iwe mwakilishi wa China bara kwenye UM, hivyo Jamhuri ya China alijiondoa.
Siku hizi uhusiano kati ya China zote mbili ni mgumu. Wananchi wengi wa Jamhuri ya China wameanza kujitazama kama Wataiwani, si Wachina tena. Lakini China inadai nchi hii ni sehemu yake.
Watu
haririWakazi ni 23,780,452 (2018), hivyo msongamano ni mkubwa sana.
Wengi wao (zaidi ya 95%) ni Wachina waliotokana na wale waliohamia kisiwani hasa kuanzia karne ya 17. Wenyeji ni 2% tu.
Kichina ndiyo lugha rasmi na ya taifa, pia lugha ya kawaida katika lahaja zake mbalimbali. Lugha za wenyeji, ambazo ni kati ya lugha za Austronesia, zinazidi kufa.
Nchi inaheshimu uhuru wa dini na wakazi wengi (81.3%) wanayo moja ya kwao. Serikali inazitambua 26.
Yenye wafuasi wengi ni Ubuddha (35.1%), Utao (33%), Ukristo (3.9%, wakiwemo Waprotestanti 2.6% na Wakatoliki 1.3%) na Yiguandao (3.5). Wenyeji wengi ni Wakristo (64%).
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Taiwan GDP". 2024.
Viungo vya nje
haririTaarifa za jumla
hariri- Taiwan entry at The World Factbook
- Taiwan Ilihifadhiwa 28 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Jamhuri ya China katika Open Directory Project
- Taiwan country profile BBC News
- Taiwan flashpoint BBC News
- Background Note: Taiwan US Department of State
- Taiwan Travel Information and Travel Guide Lonely Planet
- Taiwan's 400 years of history New Taiwan, Ilha Formosa
- Key Development Forecasts for Taiwan from International Futures
- Taiwan Encyclopædia Britannica entry
- Chinese Taipei OECD
- Wikimedia Atlas of Taiwan
Serikali
hariri- Office of the government Ilihifadhiwa 20 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.
- Office of the President
- Judicial Yuan
- Control Yuan
- Examination Yuan Ilihifadhiwa 1 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Taipei Economic & Cultural Representative Office in the US
- National Assembly Ilihifadhiwa 30 Juni 2005 kwenye Wayback Machine.
- Taiwan, The Heart of Asia Ilihifadhiwa 23 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine., Tourism Bureau, Republic of China (Taiwan)
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya China kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |