Chilombola

(Elekezwa kutoka Chirombola)

Chilombola ni kata ya Wilaya ya Ulanga katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67611.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,074 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,870 [2] walioishi humo.

Chilombola imepakana na kata za Euga, Mwaya na Ruaha.

Watu wengi wa kata ya Chilombola wanategemea zaidi kilimo cha mazao kama mpunga, mahindi, maharagwe, ufuta, kunde, mihogo.

Pia ufugaji na uvuvi unafanyika, ingawa kwa kiasi kidogo sana.

Elimu inapatikana kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha nne.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Morogoro - Ulanga DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-04.
  Kata za Wilaya ya Ulanga - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Chilombola | Euga | Ilonga | Iragua | Isongo | Ketaketa | Kichangani | Lukande | Lupiro | Mahenge Mjini | Mawasiliano | Mbuga | Milola | Minepa | Msogezi | Mwaya | Nawenge | Ruaha | Sali | Uponera | Vigoi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chilombola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.