Fuko-dhahabu

(Elekezwa kutoka Chlorotalpa)
Fuko-dhahabu
Fuko-dhahabu mkubwa (Chrysospalax trevelyani)
Fuko-dhahabu mkubwa (Chrysospalax trevelyani)
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda ya juu: Afrotheria (Wanyama wenye asili ya Afrika)
Oda: Afrosoricida (Wanyama kama tandaraka)
Nusuoda: Chrysochloridea (Wanyama kama fuko-dhahabu)
Broom, 1915
Familia: Chrysochloridae (Wanyama walio na mnasaba na fuko-dhahabu)
J. E. Gray, 1825
Ngazi za chini

Nusufamilia 2, jenasi 9:

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mafuko-dhahabu au mafuko butu ni wanyama wa familia Chrysochloridae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Bathyergidae na Spalacidae (oda Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za fuko-dhahabu zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Mafuko hawa huchimba mahandaki yao na miguu ya mbele iliyo na ukucha wa tatu ambao umevuvumulika. Vidole vya kwanza na vya nne vimebaki kama masalio na kile cha tano kimepotea. Miguu ya nyuma ina vidole vitano vyenye ngozi katikati. Macho yao hayafanyi kazi na yamefunika kwa ngozi. Masikio ni vipenyo vidogo tu.

Hali ya sasa

hariri

Miongoni mwa spishi 21 za mafuko-dhahabu, angalau 11 zipo hatarini kwa kutoweka. Sababu za msingi ni uchimbaji wa mchanga, utendaji mbaya wa kilimo, ukuaji wa miji, na kuwindwa na mbwa na paka wa kufugwa.

Spishi

hariri

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.