London School of Economics
(Elekezwa kutoka Chuo cha Uchumi London)
Chuo cha Uchumi London (London School of Economics and Political Science; kwa kawaida kifupi: LSE kwa London School of Economics) ni kati ya vyuo maarufu duniani katika elimu ya uchumi, jamii na siasa.
Muhtasari
haririChuo kilianzishwa mwaka 1895 mjini London na leo hii ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London. Hasa idara ya uchumi ina sifa za kimataifa.
Zaidi ya wakuu wa dola 39 walisoma katika chuo hiki na 8 kati yao wanashika nafasi ya mkuu wa nchi mwaka 2007. Maprofesa pamoja na waliopata digrii chuoni hapa jumla 14 walipokea tuzo ya Nobel ya uchumi, amani au fasihi.
Nafasi za kuendesha utafiti pamoja na nafasi kwa ajili ya wanafunzi huhesabiwa kati ya bora kabisa duniani.
Wanafunzi mashuhuri wa LSE
haririKati ya viongozi wa kimataifa waliosoma LSE ni
- John F. Kennedy (rais wa Marekani 1961-1963)
- Romano Prodi (waziri Mkuu wa Italia 1996-1998 na tena tangu 2006; 1999-2004 Rais wa Kamati ya Ulaya
- Mick Jagger (mwimbaji wa bendi ya Rolling Stones)
- Kwame Nkrumah (1909-1972) - Rais wa kwanza wa Ghana (1960-1966)
- Jomo Kenyatta (1891-1978) Rais wa kwanza wa Kenya (1964-1978)
- Mwai Kibaki (b. 1931) - Rais wa Kenya (tangu 2002)
Wikimedia Commons ina media kuhusu: