Romano Prodi
Romano Prodi (Scandiano 9 Agosti 1939) ni mchumi na mwanasiasa wa Italia. Aliwahi kuwa waziri mkuu wa Italia mara mbili: 1996-1998 na 2006-2008.
Profesa wa uchumi
haririProdi aliwahi kuwa profesa wa uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Bologna kati ya 1971 na 1999. Mwaka 1978 aliitwa na Waziri Mkuu Giulio Andreotti kujiunga na serikali yake kama waziri wa viwanda. Baada ya kuanguka kwa serikali hiyo mwaka 1979 Prodi alirudi Chuo Kikuu.
Waziri Mkuu mara ya kwanza
haririMwaka 1996 alipewa nafasi ya kiongozi wa ushirikiano wa "Ulivo" (yaani "Mzeituni") uliounganisha vyama mbalimbali vya kisiasa vya mrengo wa kushoto akamshinda Silvio Berlusconi na umoja wake wa kisiasa wa mrengo wa kulia akawa waziri mkuu. Akajiuzulu 1998 baada ya kuporomoka kwa ushirikiano wa Ulivo bungeni.
Kiongozi wa Ulaya
haririMwaka 1999 akachaguliwa kama mbunge wa Bunge la Ulaya akateuliwa kuwa mwenyekiti au raisi wa Kamati ya Ulaya kwa kipindi cha 1999 hadi 2004. Aliongoza Umoja wa Ulaya katika majadiliano ya kupokea nchi kumi kama wanachama wapya mwaka 2004.
Waziri Mkuu awamu wa pili
haririBaada ya kumaliza kipindi hicho akarudi katika siasa ya Italia akashinda tena uchaguzi wa bunge la mwaka 2006 dhidi ya Berlusconi. Tangu 17 Mei mwaka huo akawa waziri mkuu wa Italia mara ya pili akiongoza ushirikiano wa vyama unaoitwa "Unione" (yaani "umoja"). Serikali yake ilianguka mwaka 2008.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Romano Prodi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |