Clare Rewcastle Brown

Mwanaharakati wa Uingereza

Clare Rewcastle Brown ni mwandishi wa habari wa Uingereza anayejihusisha na masuala ya mazingira na kupinga ufisadi, ambaye alifichua kashfa ya 1Malaysia Development Berhad (1MDB). Alizaliwa katika Koloni la Uingereza la zamani la Sarawak (ambayo sasa ni sehemu ya Malaysia), ndiye mwanzilishi na mwendeshaji wa blogu ya Sarawak Report na Radio Free Sarawak ambayo imefichua ufisadi unaochochea uharibifu wa misitu na ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo hilo pamoja na mapungufu ya mifumo ya kifedha ya kimataifa inayowezesha utawala wa kifisadi. Mnamo mwaka 2015, alihamishia lengo lake kwa serikali ya shirikisho ya Malaysia na waziri mkuu wa nchi hiyo, Najib Razak. Blogu yake, Sarawak Report, ilipata umaarufu mkubwa kwa kufichua kashfa ya 1MDB, jambo ambalo lilichangia umma kutokua na imani dhidi ya serikali ya Najib ya Barisan Nasional, na hatimaye kusababisha kushindwa kwake katika uchaguzi wa mwaka 2018.. [1] [2]

Clare Rewcastle Brown
binadamu
Jinsiamwanamke Hariri
Nchi ya uraiaUfalme wa Muungano Hariri
Jina halisiClare Hariri
Jina la familiaBrown Hariri
Tarehe ya kuzaliwa1959 Hariri
Mahali alipozaliwaCrown Colony of Sarawak Hariri
MwenziAndrew Brown Hariri
Kaziactivist, blogger, founder Hariri
AlisomaLondon School of Economics Hariri

Maisha, elimu, na kazi

hariri

Rewcastle Brown alizaliwa Sarawak, koloni la Uingereza, tarehe 20 Juni 1959 na wazazi wa Uingereza, kabla ya eneo hilo kuwa sehemu ya Malaysia. Alisoma shule ya msingi katika jimbo jirani la Sabah. Baba yake, Patrick John Rewcastle, aliwahi kuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi maalumu huko Sarawak na baadaye, baada ya uhuru, akawa Kamishna wa Polisi wa Kifalme wa Malaysia huko Sabah. [3] [4] [5] Mama yake, Karis Louise Hutchings, alikuwa mwalimu wa ukunga na alisaidia kuhudumia watoto wachanga wa jamii za asili katika kliniki za mbali. Alihamia Uingereza alipokuwa na umri wa miaka minane, alihudhuria shule ya bweni ya binafsi, kisha akasoma historia ya kisasa katika Chuo cha King's College London nabaadaye akapata shahada ya uzamili katika mahusiano ya kimataifa kutoka Shule ya Uchumi ya London (LSE). [6] Alianza kazi ya uandishi wa habari kwa kujiunga na BBC World Service mwaka 1983. Baadaye alihamia kitengo cha masuala ya sasa cha televisheni ya BBC kama mtayarishaji, kisha akafanya kazi kama ripota wa Sky TV na baadaye kama mwandishi wa habari na vipindi wa Carlton Television ya ITV.

Marejeo

hariri
  1. "Malaysia's mega 1MDB scandal that brought down a prime minister", 26 July 2020. 
  2. "U.S. Seeks to Recover $1 Billion in Largest Kleptocracy Case to Date". FBI. 20 Julai 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Malaysian 1MDB scandal: How Clare Rewcastle Brown and Sarawak Report are taking on Najib Razak". International Business Times UK (kwa Kiingereza). 2016-02-18. Iliwekwa mnamo 2021-08-30.
  4. Rewcastle Brown, Clare (2018). The Sarawak Report: The Inside Story of the 1MDB Exposé. Lost World Press. ku. [photo caption on unnumbered photo pages]. ISBN 9781527219366.
  5. "The Rewcastles". commsmuseum.co.uk. Iliwekwa mnamo 2024-07-27.
  6. Rewcastle Brown 2018. uk. 60.