Clarence Ashley

Mwanamuziki wa Marekani

Clarence "Tom" Ashley (29 Septemba 1895 - 2 Juni 1967) alikuwa mwanamuziki na mwimbaji kutoka nchini Marekani, ambaye alicheza na kutumbuiza muziki wa banjo wa clawhammer na gitaa.

Clarence Ashley

Alianza kuigiza kwenye maonyesho ya mambo ya dawa katika eneo la Kusini mwa Appalachian mapema katika miaka ya 1911, na alipata umaarufu awali mwishoni mwa miaka ya 1920 kama msanii wa kurekodi na kama mshiriki wa bendi mbalimbali za kupiga gitaa.Ashley alitumia miaka ya mwisho ya maisha yake akicheza kwenye matamasha ya muziki wa kitamaduni, pamoja na kuonekana kwenye Ukumbi wa Carnegie huko New York na kwenye tamasha la Watu wa Newport huko Rhode Island .

Maisha ya awali hariri

Ashley alizaliwa Clarence Earl McCurry huko Bristol, Tennessee mnamo 1895, mtoto pekee wa George McCurry na Rose-Belle Ashley. Wale waliomjua George McCurry walimtaja kwa njia tofauti kama "mchezaji mwenye jicho moja, mfufuaji wa kuzimu, na muongeaji sana." [1] Muda mfupi kabla ya Clarence kuzaliwa, babake Rose-Belle, Enoch Ashley, aligundua kwamba mkwe wake George alikuwa mzinzi na kufanya mapenzi na wasichana tofautitofauti aliokuwa akikutana nao. George alilazimika kuondoka mjini. Rose-Belle alirudi nyumbani na baba yake, katika mwaka 1900 familia ilihamia Shouns, Tennessee, njiapanda kusini mwa mji ujulikanayo kama mji wa mlima, ambapo Enoch aliishi katika nyumba ya kupanga. Clarence alipokuwa mchanga sana, alipewa na babu yake Enoch jina la utani la "Tommy Tiddy Waddy", na hivyo kujulikana kama 'Tom'. Alipokuwa akilelewa na wazazi wa mama yake, jina "McCurry" liliondolewa na kuwekwa jina la "Ashley".

Marejeo hariri

  1. Joe Wilson, "Tom Ashley". In Greenback Dollar: The Music of Clarence "Tom" Ashley [CD liner notes]. County Records, 2001.