Dagaa
Dagaa | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dagaa-papa tumbo-laini (Amblygaster leiogaster)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Familia 5:
|
Dagaa ni jina la kawaida la samaki wa oda Clupeiformes isipokuwa spishi za familia Chirocentridae. Spishi nyingi zina majina mengine pia, kama vile kapenta, kerenge, lumbu, mbarata, mwatiko, ndakala, pata, pawali, simu, uono na usipa. Spishi kadhaa za familia Alestidae, Apogonidae, Atherinidae, Cyprinidae na Leiognathidae huitwa dagaa pia lakini majina mengine yanapendelewa. Dagaa wanatokea katika bahari zote za dunia na katika maziwa na mito mingi.
Kibofuhewa cha Clupeiformes kimeungana na utumbo kwa kifereji. Kwa kawaida hawana mrabafahamu (mstari wa ubavu, lateral line kwa Kiingereza) lakini wana macho, mapezi na magamba ambayo ni ya kawaida kwa samaki wengi, ingawa siyo samaki wote wana sifa hizi. Wao ni samaki wenye rangi ya fedha na mwili mwembamba wenye umbo la dulabu, na mara nyingi huunda makundi. Takriban spishi zote hula planktoni ambazo huzichuja kutoka kwa maji kwa matamvua yao.
Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki
hariri- Amblygaster sirm, Dagaa-papa Madoadoa (Spotted sardinella)
- Dussumieria elopsoides, Dagaa-papa Upinde-mvua (Slender rainbow sardine)
- Encrasicholina heteroloba, Dagaa-mcheli Kichwa-kifupi au Uono (Shorthead anchovy)
- Engraulicypris spinifer, Usipa wa Malagarasi (Malagarasi sardine)
- Etrumeus wongratanai, Dagaa-papa wa Bahari ya Hindi (East African round herring)
- Herklotsichthys punctatus, Dagaa-papa Mgongo-madoa (Spotback herring)
- Limnothrissa miodon, Lumbu au Dagaa wa Ziwa Tangayika (Lake Tanganyika sardine)
- Pellona ditchela, Simu koko au Dagaa-papa Mhindi (Indian pellona)
- Rastrineobola argentea, Dagaa wa Ziwa Viktoria au Mukene (Lake Victoria sardine)
- Sardinella neglecta, Dagaa-papa Mashariki (East African sardinella)
- Spratelloides gracilis, Dagaa Milia-fedha (Silver-stripe round herring)
- Stolephorus indicus, Dagaa-mcheli Mhindi (Indian anchovy)
- Thryssa setirostris, Dagaa-mcheli Taya-refu (Longjaw thryssa)
Picha
hariri-
Dagaa-papa madoadoa
-
Dagaa-papa upinde-mvua
-
Dagaa-mcheli
-
Dagaa-papa wa Bahari ya Hindi
-
Dagaa-papa milia-buluu
-
Dagaa-papa kichwa-kirefu
-
Dagaa milia-fedha
-
Dagaa-mcheli Mhindi
-
Dagaa-mcheli sharabu
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
haririDagaa kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 13 Agosti 2019 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dagaa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |