Shorobo
(Elekezwa kutoka Crinifer)
Shorobo, dura au huruvi ni ndege wa familia Musophagidae. Spishi za jenasi Corythaixoides zinaitwa gowee pia na Tauraco fischeri anaitwa kulukulu. Spishi za jenasi Corythaixoides na Crinifer zina rangi ya kijivu na nyeupe, nyingine zina rangi ya majani, nyekundu, buluu na zambarau. Shorobo ni ndege wa pekee ambao wana pigmenti ya rangi ya majani inayoitwa turacoverdin. Ndege hawa wanatokea Afrika chini ya Sahara. Hawawezi kupuruka vizuri sana lakini hukimbia juu ya matawi ya miti. Hula matunda hasa na majani na maua pia, na mara chache hukamata wadudu na makoa. Hujenga tago lao kwa vijiti na jike hutaga mayai 2 au 3. Vinda wakitoka kwa mayai, wanapambwa na malaika mazito na macho yao ni wazi tayari au karibu.
Spishi
hariri- Corythaeola cristata, Shorobo Mkuu (Great Blue Turaco)
- Corythaixoides concolor, Shorobo au Gowee Kijivu (Grey Go-away-bird)
- Corythaixoides leucogaster, Shorobo au Gowee Tumbo-jeupe (White-bellied Go-away-bird)
- Corythaixoides personatus, Shorobo au Gowee Uso-mweusi (Bare-faced Go-away-bird)
- Crinifer piscator, Shorobo Tumbo-michirizi (Western Plantain-eater)
- Crinifer zonurus, Shorobo Mkia-miraba (Eastern Plantain-eater)
- Musophaga rossae, Shorobo Uzuri (Ross's Turaco)
- Musophaga violacea, Shorobo Zambarau (Violet Turaco)
- Ruswenzorornis johnstoni, Shorobo wa Ruwenzori (Ruwenzori Turaco)
- Tauraco bannermani, Shorobo wa Bannerman (Bannerman's Turaco)
- Tauraco corythaix, Shorobo wa Knysna (Knysna Turaco)
- Tauraco erythrolophus, Shorobo Kishungi-chekundu (Red-crested Turaco)
- Tauraco fischeri, Kulukulu (Fischer's Turaco)
- Tauraco hartlaubi, Shorobo Buluu (Hartlaub's Turaco)
- Tauraco leucolophus, Shorobo Kishungi-cheupe (White-crested Turaco)
- Tauraco leucotis, Shorobo Domo-machungwa (White-cheeked Turaco)
- Tauraco livingstonii, Shorobo-pwani (Livingstone's Turaco)
- Tauraco macrorhynchus, Shorobo Domo-njano (Yellow-billed Turaco)
- Tauraco persa, Shorobo Kijani (Green au Guinea Turaco)
- Tauraco porphyreolophus, Shorobo Kishungi-zambarau (Purple-crested Turaco)
- Tauraco ruspolii, Shorobo wa Ruspoli (Prince Ruspoli's Turaco)
- Tauraco schalowi, Shorobo Kibwenzi (Schalow's Turaco)
- Tauraco schuettii, Shorobo Domo-jeusi (Black-billed Turaco)
Picha
hariri-
Shorobo mkuu
-
Gowee kijivu
-
Gowee tumbo-jeupe
-
Gowee uso-mweusi
-
Shorobo tumbo-michirizi
-
Shorobo mkia-miraba
-
Shorobo uzuri
-
Shorobo zambarau
-
Shorobo wa Knysna
-
Shorobo kishungi-chekundu
-
Kulukulu
-
Shorobo buluu
-
Shorobo kishungi-cheupe
-
Shorobo-pwani
-
Shorobo domo-njano
-
Shorobo kijani
-
Shorobo kishungi-zambarau
-
Shorobo wa Ruspoli
-
Shorobo kibwenzi
-
Shorobo domo-jeusi