Cristina Cini (alizaliwa 11 Julai 1969 huko Firenze, Toscana) ni mwanamke wa kwanza wa Italia kuwa mwamuzi msaidizi wa mpira wa miguu katika soka la Italia.

Alianza kuchezesha mechi za ligi ya Serie B katika msimu wa mwaka 2002-03, akimsaidia mwamuzi Antonio Dattilo katika mechi ya Trestina - Venezia (1-2), mnamo 14 Septemba 2002. Mnamo 24 Mei 2003, alichezesha kwa mara ya kwanza mechi ya ligi ya Serie A, akimsaidia mwamuzi Tiziano Pieri katika mechi ya Juventus - Chievo (4-3).

Mnamo 2 Julai 2012, alistaafu, akiwa na jumla ya mechi 43 akiwa kama mwamuzi msaidizi wa mpira wa miguu. [1]

Marejeo

hariri
  1. "Formazione dei ruoli arbitrali per la stagione sportiva 2012/13". 2 Julai 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-02. Iliwekwa mnamo 2023-04-02. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cristina Cini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.