Daa
Daa | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Daa-damu kutoka Ulaya (Marphysa sanguinea)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusungeli 4: |
Daa, choo au mwata ni wanyama wa bahari (spishi kadhaa kwenye maji matamu na nchi kavu) ya ngeli Polychaeta ya faila Annelida (anelidi). Spishi nyingi sana huishi katika mashapo ya sakafu ya bahari au matope ya maziwa na mabwawa, na spishi zinazoishi karibu na pwani hutumika kama chambo cha kuvulia samaki. Spishi nyingine huogelea huru majini na kadhaa zinatokea katika maeneo manyevu ya nchi kavu. Spishi zinazotumika kama chambo huitwa daa kwa kawaida, lakini inapendekezwa kutumia jina hili kwa spishi zote za Polychaeta.
Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki
hariri- Chloeia flava, Daa-moto dhahabu (Golden fireworm)
- Cirriformia tentaculata, Daa matamvua-marefu (Red thread-gilled worm)
- Drilonereis logani
- Eunice aphroditois, Daa-vamia (Sand striker)
- Eunice grubei
- Eunice leucosticta
- Eunice wasinensis
- Eupolymnia nebulosa, Daa-spageti (Spaghetti worm)
- Haplosyllis spongicola, Daa-sifongo (Sponge worm)
- Harmothoe imbricata, Daa-magamba (Scale worms)
- Marphysa macintoshi, Daa-damu wa Macintosh (Marphysa)
- Marphysa mossambica, Daa-damu wa Msumbiji
- Platynereis dumerilii, Daa-bapa (Platynereis dumerilii)
- Pseudobranchiomma longa, Daa-kipepeo mrefu (Giant fanworm)
- Rhamphobrachium chuni
- Serpula vermicularis, Daa-chokaa (Calcareous tubeworm)
- Spirobranchus giganteus, Daa Mti-wa-Krismasi, (Christmas tree worm)
- Subadyte pellucida, Daa wa Kiti cha Pweza (Subadyte pellucida)
- Tomopteris rolasi, Daa-planktoni (Gossamer worm)