Sakafu ya bahari (kwa Kiingereza seabed, sea floor, seafloor au ocean floor) ni sehemu ya chini kabisa ya bahari au, kwa lugha nyigine, ni sehemu ya uso wa dunia iliyofunikwa na maji ya bahari.

Sakafu ya bahari jinsi ilivyo kwenye mtelemko wa tako la bara kuelekea vilindi vya bahari.

Kina cha maji juu ya sakafu ya bahari kinacheza kati ya mita chache hadi takriban kilomita 11 katika mifereji ya bahari. Kwa wastani sakafu iko mita 3,800 chini ya uso wa bahari.

Maeneo ya sakafu ya bahari huchunguliwa kwa kutumia nyambizi za utafiti na siku hizi pia kwa picha na vipimo vya satelaiti. Kwenye sehemu zenye kina kidogo, hasa kwenye tako la bara, inawezekana pia kwa wazamiaji kufikia sakafu ya bahari.

Sawa na uso wa dunia barani sakafu ya bahari huwa na milima, mabonde, tambarare na volkeno. Kwa jumla maeneo mbalimbali ya sakafu ya bahari hufanana kuliko maeneo ya uso wa dunia bara kwa sababu athira za kufinyanga na kubadilisha uso wa sakafu ni chache kulingana na nchi kavu. Hapo chini ni hasa mikondo ya maji inayobadilisha uso wa sakafu tofauti na nchi kavu ambako mvua, mito, upepo na mabadiliko makali ya joto na baridi zinachangia mmomonyoko na kufinyanga uso wa nchi.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.