Daniele Rugani
Mchezaji wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Italia
Daniele Rugani (matamshi ya Kiitalia: [danjɛːle ruɡaːni]; alizaliwa 29 Julai 1994) ni mchezaji wa soka wa Italia ambaye anacheza kama beki wa kati wa klabu ya Serie A, Juventus FC na timu ya taifa ya Italia.
Alianza kazi yake katika klabu ya Empoli ya Serie B mwaka 2013, ambapo alisaidia klabu mara moja kufuzu Serie A, na kumfanya awe beki bora wa mwaka 2014 wa Serie B.
Maonyesho yake ya msimu ulimfanya aitwe kwenye timu ya Serie A mwaka 2015, na kuhamia Juventus, ambako mara moja alishinda kombe la Serie A wakati wa msimu wake wa kwanza na klabu hiyo.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Daniele Rugani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |