Darubini ya anga-nje

(Elekezwa kutoka Darubini za anga-nje)

Darubini ya angani (ing. Space observatory au space telescope) ni kifaa hasa darubini kilichorushwa katika anga la nje kwa kusudi la kuangalia na kupima violwa vya mbali kama vile nyota, sayari, galaksi na magimba mengine. Faida yake ni ya kwamba inaweza kuchungulia violwa hivi nje ya angahewa ya Dunia. Angahewa ni kama chujio inayozuia sehemu za spektra ya mawimbi ya sumakuumeme pia huwa na mwendo ndani yake unaoleta machafuko wa namna ya kuona nyota. Kwa hiyo darubini za angani zinaweza kuleta matokeo mazuri zaidi kushinda vifaa kwenye paoneaanga duniani.

Hubble ni moja ya darubini ya anga-nje mashuhuri

Darubini za angani kwa kawaida ziko kwenye obiti ya kuzunguka Dunia au zinawekwa kwa umbali ambako graviti ya Jua na Dunia inajisawazisha yaani kwenye nukta ya Lagrange. Darubini ya Spitzer inafuata obiti ya kuzunguka Jua.

Utazamaji wa nyota kutoka kifaa kilichopo angani unawezesha vipimo nje ya spektra za nuru inayoonekana na mawimbi ya redio kama vile mawimbi ya infraredi na urujuanimno ambayo yanazuiliwa na angahewa. Pia picha zinazochukuliwa nje ya angahewa ambako miale ya nuru hazipiti kwenye uchepuko wa tabaka za hewa ni bora kuliko picha zinazopigwa duniani.

Darubini za angani muhimu (si orodha kamili)

Jina Tarehe ya kurushwa Mwisho Upeo wa vipimo Isimamizi na
1968 / 1973 1977
Uhuru (SAS-1) 1970 1973 eksirei NASA
Orbiting Astronomical Observatory 3 (Copernicus) 1972 1981 urujuanimno, eksirei NASA
COS-B 1975 1982 gamma ESA
International Ultraviolet Explorer 1978 1996 urujuanimno NASA, ESA, SERC
Infrared Astronomical satellite 1983 1983 infraredi
Astron (satelaiti) 1983 1989 urujuanimno, eksirei Umoja wa Kisovyeti/Ufaransa
EXOSAT 1983 1986 eksirei ESA
Ginga 1987 1991 eksirei ISAS
Cosmic Background Explorer (COBE) 1989 1993 mikrowevu NASA
Hipparcos 1989 1993 nuru inayoonekana ESA
ROSAT 1990 1999 eksirei DLR
Hubble 1990 nuru inayoonekana, urujuanimno, infraredi NASA, ESA
Compton gamma Ray Observatory 1991 2000 gamma NASA
Yohkoh 1991 2001 eksirei ISAS
Extreme Ultraviolet Explorer 1992 2001 urujuanimno NASA
Advanced satelaitie for Cosmology and Astrophysics (ASTRO-D) 1993 2000 eksirei ISAS
Infrared Space Observatory 1995 1998 infraredi ESA
Solar and Heliospheric Observatory 1995 nuru inayoonekana, urujuanimno NASA, ESA
Rossi X-ray Timing Explorer (RXTE) 1995 2012 eksirei NASA
BeppoSAX 1996 2002 eksirei ASI
Far Ultraviolet Spectroscopic Explorer 1999 2007 urujuanimno NASA
Chandra (darubini) 1999 eksirei NASA
XMM-Newton 1999 eksirei ESA
Wilkinson Microwave Anisotropy Probe (WMAP) 2001 2010 mikrowevu NASA
Integral (satellite) 2002 gamma ESA
Galaxy Evolution Explorer 2003 2013 urujuanimno NASA
Spitzer darubini ya anga-nje 2003 infraredi NASA
MOST (satellite) 2003 CSA
Swift (satellite) 2004 gamma NASA
ASTRO-E (Suzaku) 2005 eksirei JAXA
ASTRO-F (Akari) 2006 2011 infraredi JAXA
COROT (darubini ya anga-nje) 2006 2013 nuru inayoonekana CNES/ESA
AGILE 2007 gamma ASI
Fermi gamma-ray Space Telescope 2008 gamma NASA
Kepler (darubini ya anga-nje) 2009 2013 nuru inayoonekana, infraredi NASA
Planck (darubini ya anga-nje) 2009 2013 mikrowevu ESA
Herschel (darubini ya anga-nje) 2009 2012 für HFI infraredi ESA
Wide-Field Infrared Survey Explorer 2009 2011 infraredi NASA
RadioAstron (Spektr R) 2011 mikrowevu Idara ya stronomia ya Taasisi ya Lebedew kwa Fizikia, Moskwa[1]
NuSTAR 2012 eksirei NASA
NEOSSat 2013 nuru inayoonekana CSA
Gaia 2013 nuru inayoonekana ESA
ASTRO-H (Hitomi) 2016 eksirei JAXA, NASA, ESA, CSA
Hard X-ray Modulation Telescope (HXMT) 2017 eksirei CNSA
James Webb (darubini ya anga-nje) 2021 infraredi NASA, ESA, CSA
Public Telescope (PST) 2019 (inapangwa) nuru inayoonekana, Ultraviolett (urujuanimno) astrofactum[2]
ASTRO-1 Telescope 2020 (inapangwa) nuru inayoonekana, Ultraviolett (urujuanimno) BoldlyGo Institute[3][4]
Euclid (darubini ya anga-nje) 2020 (inapangwa) nuru inayoonekana, nahes infraredi ESA
  1. RadioAstron Ilihifadhiwa 31 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine., Lebedew-Institut für Physik, abgerufen am 30. August 2011.
  2. Ein privates darubini ya angani für Amateure und Profis
  3. "Astro-1 Space Telescope". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-26. Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
  4. Corning Donates $1.8 Million in Parts for ASTRO-1 Telescope