Daudi Mwangosi

Muandishi wa Habari wa Tanzania


Daudi Mwangosi (1972Septemba 2, 2012) alikuwa mwandishi wa habari wa kituo binafsi cha runinga cha Chanell Ten, Mwangosi aliuliwa katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa ,wakati wa maandamano ya wafuasi wa Chadema.[1][2]

Daudi Mwangosi
Amezaliwa 1972
Busoka mkoani Mbeya.
Amekufa 2 Septemba 2012
kijiji cha Nyololo
Nchi tanzania
Kazi yake mwandishi wa habari wa kituo binafsi cha runinga cha Chanell Ten
Cheo mwenyekiti wa waandishi wa habari Iringa.
Kipindi mwaka 2015
Ndoa ana mke na watoto wanne
Watoto 4
Mahusiano mke

Taaluma hariri

Daudi Mwangosi alianza kazi ya uandishi wa habari mnamo mwaka 2015 katika kituo cha runinga cha Chanell ten ambacho ni kituo cha habari binafsi na mnamo mwaka 2011 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa waandishi wa habari Iringa.

Kifo hariri

 
Nyololo iko nje ya Iringa, Tanzania. Inaonyeshwa hapa kuhusiana na mji mkuu wa Dodoma.

Mnamo 2 Septemba 2012, Daudi Mwangosi aliuliwa katika kijiji cha Nyololo wakati akifuatilia ufunguzi wa ofisi ya Chadema, chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Mwangosi alikuwa akifuatilia tukio la ufunguzi huo na wakati huo polisi walikuwa wamezuia mkusanyiko wa wafuasi wa chama hicho cha siasa kwa sababu ilidaiwa kuwa kinyume cha sheria.[3], Mwangosi aliuliwa kwa kupigwa bomu wakati akijaribu kumsaidia muandishi mwenzake Godfrey Mushi alokuwa muandishi wa gazeti la Nipashe .[4][2][5]

Mwangosi aliaga dunia baada ya kupigwa [bomu la machozi] tumboni kwa karibu zaidi na kusababisha mauti yake, askari alohusika na mauaji yake alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano gerezani.

Mwangosi aliaga dunia akiwa na umri wa miaka arobaini, aliacha mke na watoto wanne.[6], alizikwa katika kijiji cha Busoka mkoani Mbeya.[7][5]

Marejeo hariri

  1. "Tanzanian TV journalist killed", September 3, 2012. 
  2. 2.0 2.1 Prominent Tanzanian journalist killed in scuffle with police. Committee to Protect Journalists (September 4, 2012).
  3. Team to investigate killing of Dar TV reporter - News. nation.co.ke. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-09-06. Iliwekwa mnamo 2013-10-05.
  4. Ng, Fumbuka (September 4, 2012). Tanzanian journalist killed reporting police-opposition clash. Reuters. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-03-18. Iliwekwa mnamo April 22, 2017.
  5. 5.0 5.1 Prominent Tanzanian journalist killed in scuffle with police -. Committee to Protect Journalists (2012-09-04). Iliwekwa mnamo 2013-10-05.
  6. Daudi Mwangosi. Committee to Protect Journalists (September 2, 2012).
  7. UjenziOnline. MWANDISHI DAUDI MWANGOSI AZIKWA KIJIJINI KWAKE....
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daudi Mwangosi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.