David Blaine (David Blaine White; alizaliwa Brooklyn, New York City, 4 Aprili 1973) ni mfanyamazingaombwe wa Marekani. Ameweka na kuvunja rekodi kadhaa za dunia.

David Blaine

Amezaliwa 4 Aprili 1973
Brooklyn
Nchi Marekani
Kazi yake mfanyamazingaombwe

Maisha ya awali na ya binafsi

hariri

Blaine alizaliwa na kukulia huko Brooklyn. Baba yake, William Perez, alikuwa askari katika vita vya Vietnam. Mama yake, Patrice Maureen White, alikuwa mwalimu wa shule.

Alipokuwa na umri wa miaka minne, aliona mazingaombwe yakifanywa katika maonyesho ya mazingaombwe barabarani, akawa na hamu ya somo hilo.

Baada ya kukua, alinyanyuliwa na mama yake. Alihudhuria shule nyingi. Alipokuwa na umri wa miaka kumi, mama yake aliolewa na mtu mwingine, na familia hiyo ikahamia Little Falls, New Jersey.

Blaine ana ndugu aitwaye Michael James Bukalo. Alipokuwa na umri wa miaka 17, alihamia Manhattan.

Blaine alifunga ndoa na Alizee Guinochet. Wana binti mmoja, Dessa, ambaye alizaliwa Januari 2011.

Tangu mwaka 1997 na katika maisha yake yote, Blaine amekuwa akifanya aina zote za stunts. Baadhi yao hujumuisha:

  • Mazingaombwe wa mitaani na Mtu wa uchawi 
  • Kuzikwa mzima
  • Kuganda kwa muda
  • Sulisuli   
  • Kuelea hewani   
  • Zamishwa kwenye maji akiwa mzima
  • Kupigwa shoti na mamilioni ya volti   
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Blaine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.